Monday, October 15, 2007

Ze comediiiiiiii noma! Ferouzi chali nakwambia!

KUNDI la Ze Comedy limempiga bao msanii Ferooz kwa kutoa video ya wimbo wake wa ‘Bosi’.
Ze Comedy wakiongozwa na Masanja Mkadamizaji, wiki iliyopita waliibuka katika kipindi chao cha kila Alhamisi na video ya wimbo wa ‘Bosi’ ulioimbwa na Ferooz na kuwashirikisha Juma Nature na Solo Thang ambaye sasa anaishi Ireland Kaskazini.

Ferooz anasema kuwa hakutoa video hiyo kwa sababu kampuni iliyomtengenezea ilidai kuwa kulitokea matatizo katika kompyuta aliyohifadhiwa na kusababisha iungue wimbo huo ukiwa ndani.

“Sikuwa na ujanja na nikaona ni kazi tena kuanza kuwakusanya Nature na Solo ambao walitumia muda wao. Lakini pia baadaye Solo akaondoka kwenda Ulaya, lakini bado nilikuwa na wazo la kutengeneza tena video yake.

“Lakini jamaa nimeona wametoa video ambayo ukiangalia utaona ni wabunifu, si tu kwamba wameniwahi na kufanya video nzuri hata kabla yangu. Lakini wamejitahidi kuonyesha ni kitu waliochokikubali na kukifuatilia. Nimewakubali sana,” anasema.

Alipoulizwa Nature :Hata video yao imetengenezwa vizuri sana, hisia zao walikuwa utafikiri wao ndiyo Nature, Ferooz au Solo. Wamefanya vizuri mimi wamenifurahisha,” anasema Nature.

1 comment:

Epukeni Utumwa wa Akili said...

oyaaa mbona husemi masuala ya Mwanamkude?