Friday, October 12, 2007

Waacheni wazungu wawatie adabu!

BONGO au kwa Kiswahili inavyoitwa Darisalama ni jiji lililojaa Wajanja naWajinga wasio na idadi.Kwani wewe bado hujajua kwamba ujanja ukipitiliza unakuwa ushamba halafuunaishia kwenye ujinga?shauri yako.Kama hutaki basi.

Jiulize kwanini kila leo unawakuta jamaa wengi wakiwaDada zetu wakiangua kilio baada ya kuuziwa simu feki huko chini ya minaraUswazi.Sio hao tu, ebu jiulize hao wanaliwa kwenye kamari na hizo Karata tatuhuko Mnazi Mmoja na Karume.

Waache hao,hujawaskia hawa 'wanaoshikwa masikio' na madalali na kuuziwachumba kimoja watu saba huko Mwananyamala au mpaka nikutajie hawawanaoutwika na kuzimika kaunta wakidhani wanamkomoa 'Mama Muuza' kamawanavyofanya kwenye Mataputapu Nyumba za Kota?.Tuwaache hao.

Saa kidogo zijazo wateule waliokuwa wamefunga watafunguliana kusherekea sikukuu ya Pasaka.Kila kitu kwao kitakuwa fasta na ndio muda muafaka wa kuminya Ubwabwa kwaukubwa wa kinywa chako hata na tumbo lako ambalo lilikuwa likijazwa kwakikomo kwa majuma kadhaa yaliyofikia tamati.

Wapo jamaa fulani fulani ambao Mzee wa Kutibua aliwafuma wakiminya 'sosila kufa mtu' kwenye 'chobisi' moja lakini ameamua kuwasitiri ila'atawatonya' kiaina endapo atajumuika nao huko uswazi walikomualika kwenye'Debe'.

Lakini wakati mchakato huo ukiendelea,jamaa fulani wamekuwa adimu kwenyemaskani zao baada ya watoto kuja juu wakidai viwalo vya bei juu. Ndiomambo ya Pasaka hayo, kama huna hela inabidi uwe mtulivu.Uwe mtulivu na kusikiliza maelekezo toka kwa mama watoto lakini usione soolitakapokuja zoezi nyeti la kufungiwa mtoto mgongoni.

Lakini yakiachwa hayo hii tabia ya baadhi ya viongozi kuwaogopa na penginekuwabeba baadhi ya wachezaji wa hizo klabu hususani za Simba na Yanga limekuwa kero na mjadala miongoni mwa mashabiki kwa sasa.

Hali hiyo imeonekana na kuanza kutafsiriwa hivyo kutokana na matukioyaliyotokea wiki kadhaa zilizopita mpaka leo hii kwa baadhi ya wachezajikwenye klabu hizo.Wachezaji hao ambao wengi ni mastaa wa kigeni na kizalendo katika klabuhizo wamekuwa wakionyesha utovu wa nidhamu kwa kuchelewa kuripotiwamazoezini pamoja na kutofuata maelekezo ya makocha wao wa kigeni 'Wazungu'kiufasaha.

Miongoni mwa wachezaji hao wamekumbana na adhabu kadhaa huku wenginewakiwa bado wanatafutiwa njia ya kuwaadhibu ili iwe fundisho.Lakini ukiangalia kiundani suala hilo viongozi wa klabu hizo ndio wamekuwawakihusika na kuwapa vichwa wachezaji hao baada ya kushindwa kuwachukuliahatua zinazostahili.

Licha ya kwamba baadhi ya viongozi hao wengi wamekuwa hawahudhuriiprogramu za mazoezi kuona nini kinachofanyika lakini hata wanapopewataarifa kwamba mchezaji fulani hajahudhuria mazoezi wamekuwa hawachukuihatua yoyote na badala wamekuwa wakiharakisha 'kuropoka' kwenye vyombo vyahabari kwamba fulani anaumwa.

Wakati wachezaji hao wamekuwa wakionekana kwenye baa maarufu nyakati zausiku wakiponda raha huku wakidai kuwa wanasubiri mazoezi yachanganye.Labda ni ukweli kwamba pengine ni kutokana na umaskini wa fikra nakiuchumi unaowapa wasiwasi kwamba endapo wakichukua hatua kali zakuwasimamisha mastaa hao na timu ikiyumba wanaweza kupinduliwa nakuondolewa kwenye nafasi zao na wanachama kabla hawajatimiza masilahi yao.

Viongozi hao wamefikia hata hatua ya kutumia vyombo vya habari kudanganyaumma wa mashabiki hata makocha kwamba wachezaji watajiunga na kambi mudamfupi, wakielewa fika halisi ilivyo kabla ya ukweli kuwekwa hadharani palewachezaji husika wanaposimamishwa na makocha hao.

Hali ya kuwa karibu na kubebwa na viongozi imekuwa ikiwachanjia kuwaharibuwachezaji hao ambao wengi hupotea katika ramani ya soka baada ua mudakutokana na kujiona kwamba wanaweza na wako juu ya kila kitu.

Licha ya kuishi maisha ya chini lakini wamefikia hatua ya kuamini kwambakutokana umaarufu wao walioupata katika mechi kadhaa kwenye uwanja waTaifa wanaweza na hawahitaji kupoteza muda kufanya mazoezi.

Pengine inawezekana ni kutokana na upeo mdogo na elimu finyu kwa baadhi yawachezaji kama walivyodai baadhi ya makocha na ndio maana mastaa haowanashindwa kuelewa kwamba Simba, Yanga au Moro United haupaswi kuwakikomo cha maisha yao kisoka.

Awali kuanzia ngazi ya timu ya Taifa mpaka katika klabu zao walizoweakuwaonea makocha Waza
lendo ambao mara kadhaa kama walivyo viongoziwalikuwa wakisita kutoa maamuzi makali kwa kuhofia kujiingiza kwenyemigogoro na kikundi au viongozi fulani ambao walikuwa na mamlaka.

Lakini kwa hali ilivyo viongozi na wadau mbalimbali wanapaswa kuachaushabiki pembeni na kuwaachia wazungu kufanya kazi yao kama kuna kweliwanataka maendeleo na kuisogeza Tanzania huko kwa wanaojua mpira.

Muda wakuendekeza majina umekwisha tuache wanaojua tuliowapa makali waangalieviwango.Maamuzi yaliyochukuliwa na baadhi ya makocha hao wiki hii nayaunga mkonohuku nikiwasihi kutosita kushusha rungu popote panapoyumba na kumuadhibuyoyote anayekwenda kinyume na utaratibu uliowekwa.

Naamini kwamba nidhamu ya uwanjani pamoja na kufuata maelekezo ndiyo vitupekee vitakavyofanya wachezaji wetu kung'ara na kuonekana nje ambako kunasoka lenye maslahi zaidi.Mastaa wa Kibongo wanapaswa kufungua macho na kuelewa kwamba kuchezaSimba, Yanga au kumiliki gari siyo mwisho au mafanikio.

Mnapaswa kuwa namalengo ya mbali tuwaone waliko kina David Obua, Denis Oliechi, DenisOnyango au Donald Mariga.Wangapi wamejulikana Tanzania? angalieni waliko na mtafakari, 'Ustaa' wauwanja wa Taifa hamjaanza nyinyi,msivimbe vichwa. Kila mmoja azingatiekwamba enzi zinapita.

Ipo haja ya kufanya mambo kisomi na mnaweza kufika mbali endapo mkitumiana kuzingatia wanachokuambieni hao wazungu. Au vipi bwana, Ni hayo tu!

No comments: