Friday, November 30, 2007

Angetile naye alikuwepo


Mmoja wa washirika wa Mzee wa Kutibua Angetile Osiah(anayeanguka) akishindwa kuhimili vishindo kwenye tamasha la Waandishi lililofanyika hapo Dar

Monday, November 26, 2007

Ayaa..! Anaanguka hata boli haijafika


Kipa wa timu ya Wanawake wa Zanzibar, Zanzibar Heroes iliyopigwa bao 17-0 na Twiga Stars kwenye uwanja wa Taifa wa zamani wenye nyasi bandia. Hawa mademu walikiona cha moto, eti kocha anadai uwanja umewazingua eti halafu walilala kwenye jahazi.

Nyie ni watu muhimu sana ingawa mlikuwa mnaniua mida fulani


Nahodha mstaafu wa Taifa Stars, Mecky Maxime akiaga waandishi wa michezo katika mechi maalum ya kumuaga iliyoandaliwa na TFF siku fulani zilizopita. Jamaa alifunika kinoma, haijapata kutokea Bongo

Friday, November 23, 2007

"Leaders of conflict and gate collection"

WASHIKAJI mambo vipi hapo! Mwanenu nipo freshi kimtindo ingawa bongo kimechafuka kinoma wanangu. Joto kichizi wenye ngozi za vyura tu ndio wanaopeta.

Sijui ndio kiama chenyewe kinaanza kubipu bipu kiaina maana wenye jiji letu hatuelewi elewi jinsi ngoma inavyovuma kila panapoguswa hali si shwari.

Ingawa mambo fulani ni shwari wanangu wa Lugalo soo soo.. kabisa! Sijui ni ushamba au labda kwa vile ni mara kwanza kuwaibukia ebu tuwachukulie ndio fasheni.

Ngoja sasa nikupe ishu yenyewe! Mzee mzima kama kawa mambo ya kujirusha mitaa ya Bongo wikiendi siunajua ndio zake? Sasa wikiendi hiyo iliyopita masela kama saba hivi wenye nyadhifa zao wamejimwaga naiti klabu moja hapa mitaa ya Lugalo kama unaenda Tegeta. Wenyewe siku hizi wanaita Bondeni.

Wadau wakamuendea hewani Mzee mzima nikaibuka eneo la tukio tayari kushusha kitu sehemu fulani huku ukihudumiwa kama ‘Presidaa’ kutokana na unyeti wako kwenye eneo la tukio ambalo wamo jamaa wenye minoti yao ya kusumbua tawni fulu taimu.

Kuna makelele mengi humu ndani lakini baadae jinsi muda unavyokwenda unakuja kugundua kwamba kuna kikundi kingine cha jamaa kama sita kwa nyuma yenu ambao karibu wote ni kutoka kwenye hii jamii ya jamaa fulani(ya kanda ya ziwa wananihii…) ambao wanajifanya Inglishi ni sehemu ya laifu yao toka Kileji.

“Ofukozi Rwego (Rwegoshora) mpe coldi wani, halafu athazi ai don rimemba” ni kauli ya mmoja wa hao jamaa kwenye hiyo meza iliyojaa kina Rwechungura, Kaijage na wengine wengine (nimewasahau).

Baadaye kidogo wameshaanza kuzungukwa zungukwa na viumbe fulani (viburudisho wenyewe wanaviita).Ghafla huko kwenye dansini floo Dijei akaweka “Hapo vipii..” ya huyu mwanabongofleva mnayemuita Profesa nanihii…Jei.

Jamaa wawili wakaibuka zao kwenye dansin floo kuyarudi mangoma, hapo ndipo ishu iliponoga sasa jamaa walikuwa wanakata zao Tusker na Nondo sijui ndio ubrazameni wenyewe jamaa (Rwego) kachomoka kaunta fasta kaibuka chukua zake hiyo nanihii ya chupa ya kijani… Bavaria na ufunguo wa gari kaenda kuyarudi.

“Kinda gateni mpaka chuoni kikuu longi taimu kwa machizi na masista duu…” ndivyo anavyokwenda sambamba na vesi za huo mziki, huku akiwa katikati kabisa ya masela kibao(hiyo ni naiti kali). Wanaomfahamu wanapigwa butwaa kwa jinsi anavyonyanyua juu Bavaria na ufunguo wa gari hawaelewi elewi. Wengine wanafikiri labda kashinda kwenye promosheni hapo nje dakika kadhaa zilizopita ndio anasherekea.
Lakini jamaa zake wanaoendelea na kilaji mezani wanamsanifu tu “Cheki jamaa ayah…! Kashaachana na hii sasa ana Bavaria siumeona mikono ile? Mwingine anayeonekana kumfahamu vilivyo akadakia “Hamna hiyo atakuja kuinywa sianamtaka Eliza pale (ananyooshea kidole meza nyingine) anataka aone kwamba na yeye matawi halafu na usafiri haumpigi chenga”.

Duh! Hivi kumbe bado hizi staili bado zipo? Duh! Ndio matatizo ya kuvamia jiji la watu sasa hata kama umepiga skuli bado wakuja tu.

Lakini wanangu ebu ngoja kidogo tuachane na Rwego tucheki na ishu zingine huko Dasilamu mjini. Nimeskia kuna ‘Maprofesa’ wamemwaga wino tayari kutoa ‘lekcha’ Jangwani.

Huyo bosi nimebonyezwa anaitwa Condic Dusan na msaidizi, Solokoviskiii na naskia wameshapewa rungu na tayari kufanya baadhi ya ishu ili kuhakikisha neksti raundi ya Ligi Kuu kinaeleweka Jangwani. Lakini Wekundu wataachia hilo kopo la ubingwa? Simo!

Kitendo cha Yanga kuleta makocha hao raia wa Serbia ni changamoto kubwa katika soka la Tanzania ambayo inastahili kuigwa na klabu zote za Ligi Kuu ili kuinua kiwango na kubadili taswira ya soka la Bongo.

Kama ilivyo kwa wadau wengine wa Bara, naungana na wadau wengine ambao wamekuwa wakisema kwamba huenda kukawepo na changamoto kubwa kwenye Ligi haswa kutokana na uzoefu, rekodi na utaalam wa makocha hao ambao wametamba na klabu kadhaa maarufu za Afrika ya Kati na Magharibi.
Si suala la kupongezwa tu. Uongozi wa Yanga unapaswa kuacha ubabaishaji nikiwa namaanisha kwamba unapaswa kutoa ushirikiano na sapoti ya kila aina kwa makocha hao.Vinginevyo muda si mrefu watapotea tena kama walivyopotea wengine, wala hakuna atakayeshangaa.

Hao jamaa msiwageuze wadoli kwamba mmewaleta ili kujionyesha kwamba mnaweza au mna jeuri ya fedha haisaidii!

Hii kauli aliyokuwa akipenda kuitumia huyu kocha Mserbia Sredjoviv Milutin ‘Micho’ kwamba Yanga ina baadhi ya viongozi ambao ni “Leaders of Conflict and gate collection (viongozi wa migogoro na mapato ya milangoni)” ndio moja kati ya sababu zilizomfanya akashindwa kufanya mambo yake naamini bado ina ukweli ndani yake.

Sishawishiki kuamini kwamba hali hiyo imekwisha ndani ya Yanga kwa kipindi hiki cha miezi michache tangu Micho ambaye alikuwa amezoea mazingira ya ‘kiswahili’ atimke Jangwani.

Viongozi wenyewe kwa wenyewe wanapaswa kuhakikisha kwamba kila mmoja anawajibika kwa nafasi yake na hata kama ikiwezekana ziwepo kamati ndogondogo za watu makini ambao watapewa majukumu ili kuwarahishia kazi hao makocha wa kigeni.

Kuwa mzungu si kujua kila kitu, na si lazima kila kitu afanye Mwenyekiti au Katibu huu ni wakati wa mgawanyo wa majukumu. Si mtu unakaa Dar es Salaam wiki nzima wala hujui ilipo timu halafu unaskia inacheza Mbeya jumamosi unakwea pipa Ijumaa kwenda kusimamia mapato na baadae unapotea kwenye mazingira ya utatanishi.
Ebwana habari ndio hiyo! Mida basi masela.

Friday, November 2, 2007

Hii ya Nsajigwa na Ivo ni kafara

HEE..! Washikaji ndio Novemba hilo ndani ya nyumba kama masihara vile, wazee wazima ndio tunazidi kwenda eji tu kiutani utani mara unakuwa zilipendwa.

Ndio muda wa mahesabu unakaribia wanangu na mambo ya minuso minuso ya klithmasi araundi ze kona kazi kwenu sasa, ila kazi ipo unaweza kujikuta ukijibinafsisha hivi hivi.

Mambo yako kwenye mstari kiaina kwa Mzee wa Kutibua na angali akidunda uraiani kwa jeuri ingawa jua la Bongo linazingua upara wake. Si unajua aliamua kulikwaruza baada ya vinyweleo vyeupe kuanza kumnyemelea?

Ngoja nikumegeeni kwanza hii! Siku kama nne hivi zilizopita Mzee mzima niliibuka kwenye Kabaa fulani hivi mitaa ya Keinyama hapo, kwa mualiko wa mzito wa mdau fulani wa muziki wa bongo.

Siunajua tena mwanangu sehemu kama hizo, kilaji na mambo fulani fulani si ya kuuliza? Kwenye meza wapo washikadau kama wanne hivi.(ukijiskia waite kwa majina yao ya serikali.. Shekigenda, Babuu, Tesha na huyu wa mwisho nani huyu … Lucas).

Usimhesabie huyo Byarugaba ambaye alianza kutwanga nanihii..Kesto tangu mida ya lanchi alipoenda kwenye Eitimu akakuta Mpunga wa mwezi tayari umeshajaa. Yeye tayari kashazimia kitaambo, kaegemea kiti. Kinachotoka mdomoni ni kauli moja tu “…mmhh!”.

Walioko kwenye meza ya Mzee wa Kutibua ni wazito na jamaa fulani fulani huku pembeni shingo ni nyingi zinahaha kuangalia mchakato unavyokwenda, pengine ni kutokana na mijusi mizito waliyotinga washikadau ambayo kwa kawaida ya kiwanja tulichopo inahesabika au wakati mwingine haipo kabisa.

Ghafla huku nyuma kaibuka jamaa (rapa wa bendi moja hapo kinondoni) wa bendi maarufu ya Bongo kaanza kutoa salamu akiwa mita kama mia hivi “Pedeshee Shekii…, Pedeshee Shekii…” Tesha akasemaa ohooo… “kimechafuka, mtu wa mizinga huyo kashavamia, hakawii kugeuza steji hapa”

Jamaa kama vile kazilalia sana jana anavyoonekana halafu bigi chachaa mifukoni, kabla ya kupiga mzinga dada nanihii ambaye amekulia ng’ambo ya bahari (Mkunazini) kashafika karibu akamhudumia, jamaa si akaanza kuzichapa kwa hasira kama anakomoa!

Kafyonza hizo wanazoita nondo kama nane ivi ndani ya dakika chache, hajui kama kuna mnene aliyemtengea fifte ya kumkomesha, ameanza ya tisa tu hoi ngoma ikaanza kuzomea sakafu.

Ayaah…! Aibu.. watu wote mikono mdomoni wanashangaa, mambo si mambo mtu mzima kashaharibu faragha hakieleweki tena wala hata macho hataki kufungua. Kwa umbaalii anasema eeehh.. eehh! Mwanangu aibuu… watu wamebeba kama nanihii.

Lakini..! Ebu ngoja tuchenji chaneli kwanza, siku siyo nyingi sana Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa wamefungiwa na klabu hiyo miezi sita kutokana na mambo kibaaoo moja wapo likiwa ni madai ya hujuma na utovu wa nidhamu.

Wachezaji hao wanadaiwa kuhujumu timu hiyo ikafungwa na Simba 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Bara wiki sio nyingi zilizopita huko Morogoro na baadae kutoroka kambini bila taarifa kitendo kilichotafsiriwa kama utoro kazini na utovu wa nidhamu.

Wadau wa soka ambao hawafungamani na upande wowote walionyesha kushangazwa na kitendo cha kundi la mashabiki wa Yanga kumvamia na kumpiga vibaya Mapunda baada ya mechi hiyo kwa kile walichodai kuwa aliwafungisha, huku wachezaji kadhaa nao wakiambulia matusi na wengine wakitembea si mita nyingi na Polisi wakutuliza ghasia.

Lakini cha ajabu na ambacho kinashangaza wengi Ivo angeweza hata kufa kwa ajili ya makosa ya kibinadamu ya sekundu moja tu akiwa langoni. Kwanza hakuna kiongozi yoyote wa Yanga aliyeonyesha ubinadamu kwa kuibuka na kumnusuru Ivo alivyokuwa akipambana na mashabiki je? Kama si Polisi waliofanya jitihada za makusudi nini kingetokea kwa kipa huyo wa timu ya Taifa.

Achana na hilo, viongozi hao hao ambao ndio wanaowajibika na usalama wa mchezaji mbali na kwamba hata kambini hakuna aliyefika kumjulia hali kibinadamu baada ya mchezo huo, hakuna pia ambae aliyekuwa akijali hali ya vitisho kwenye simu na mitaani alivyokuwa akipata mchezaji.

Sasa katika mazingira kama hayo, unategemea mchezaji aendelee tu kuendelea kuishi kambini na kuitumikia timu katika mazingira gani wakati hata kocha mwenyewe, ameshanukuliwa na vyombo vya habari akidai kwamba ni kosa la kipa limewanyima ushindi?

Hali hiyo ndio iliyowakumba na wachezaji wengine kama Nsajigwa na Amir Maftah ambao waliamua kuingia mitini. Ingawa Maftah hajafungiwa kwa madai kuwa bado hajaitwa kujieleza.

Lakini kinachoonekana ni kwamba viongozi wa Yanga wamewahukumu wachezaji hao kwa kutumia propaganda za kiuongozi zaidi na hawana sababu za msingi za kisomi ambazo ukiwakurupusha hata sasa wanaweza kukuambia ukaridhia.

Mazingira hayo ndio yanafanya wadau wa soka na wenye upeo mkubwa kwenye masuala ya kiuongozi waamini kwamba wachezaji hao wametolewa kafara ili kulinda maslahi ya viongozi mbele ya wanachama, ambao wiki chache zilizopita walikuwa wanavurugana wenyewe kwa wenyewe.

Hakuna mwanamichezo asiyeelewa kwamba mpira ni mchezo wa makosa na huwezi kuwa juu siku zote ndio maana kukawa na usiku na mchana, hakuwezi kuwa mchana tu siku zote. Mbona Lehman wa Arsenal amefungwa mabao ya kizembe mechi kama nne mfululizo hatujaskia amesimamishwa miezi au hata kutozwa faini.

Paul Robison wa Totenham Hotspurs ambaye kila mechi anafungwa bao la kizembe mbona hatujaskia kaadhibiwa? Tena kasajiliwa kwa mabilioni sembuse Ivo wa Tukuyu ambaye hata glovu za mazoezi ananunua kwa machinga Kariakoo?

Achana na hao Richard Micah beki tegemeo wa Manchester City (kama ilivyo Nsajigwa kwa Yanga) ambaye yeye pamoja na wenzake wamefanywa uchochoro wakapigwa 6-0 na Chelsea stanfodi briji, angekuwa Yanga ingekuwaje?

Sipingi kwamba uongozi unaweza kumpa mchezaji adhabu kama muajiri na muajiriwa lakini si hii ya miezi sita ya Ivo na Nsajigwa iliyotolewa na uongozi wa Madega, ni kuua vipaji vya wachezaji na ni ubabe pia, kufungwa na Simba sio mwisho wa Dunia. Msiendekeze kelele za mashabiki wachache ambao wana maslahi yao.

Achana na umuhimu wao Taifa Stars, inawezekana kuna makosa yamebainika kwa utashi wa viongozi lakini kwanini wasingepigwa faini au kukatwa mshahara kwa miezi hata miwili kama inavyofanywa kwenye nchi zilizoendelea kuliko kutoa adhabu kama tunazoshuhudia ambazo siogopi kusema ni za kizamani na za kienyeji.

Halafu isitoshe viongozi hao hao wanakwenda Tiefuefu kuomba kipa wao aliyefungiwa mechi sita, Benjamin Haule afunguliwe ili wamtumie kwani ni hatari kubakiwa na kipa mmoja (Jackson Chove) ambae baadhi wanadiriki kumuita “namba tatu”. Kwani wakati mnamfungia Ivo hamkujua hilo na huyo?

Imefika wakati viongozi wa klabu za Tanzania kubadilika kifikra na kufanya mambo kisomi badala ya kutumia propaganda. Siwafundishi wajomba hizo ni salamu zangu kwenu.

Maximo sawa bwana-Ndabila


MSHAMBULIAJI tegemeo wa Prisons, Yona Ndabila amesema hana bahati na timu ya Taifa na wala hadhani kwamba anaweza akawemo katika miaka ya hivikaribuni.

Kauli ya mchezaji huyo imekuja siku chache baada ya kocha Marcio Maximo kutangaza kikosi cha Chalenji huku akiwa hayumo licha ya wadau wengi kushinikiza awemo.

“Timu mi naona ni nzuri, lakini mi naona kama sina bahati kabisa kipindi hiki kwa jinsi mambo ninavyoyaona,”alisema mchezaji huyo mwenye mabao manne kwenye Ligi Kuu ya Bara inayoendelea.

“Wakati huu ndio naona nipo kwenye fomu sana na ndio ilikuwa kipindi changu cha kulitumikia taifa kwa kila hali.

“Lakini ndio hivyo, labda ipo siku hii ni kazi yangu ngoja tupambane na Ligi Kuu kwanza tuone,”aliongeza mchezaji huyo mfupi kiasi mwenye maneno mengi.

Wa mnyama saba hawamo kambini

WACHEZAJI saba tegemeo wa Simba ya Dar es Salaam hawamo kwenye kambi ya mazoezi ya timu hiyo mjini Morogoro.

Simba yenye pointi 15 ikishikilia nafasi ya nane inacheza na Polisi Dodoma kesho mjini Dodoma katika mechi ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara.

Habari toka ndani ya kambi hiyo zinasema kuwa wachezaji hao watano kati yao waliondoka kambini juzi mchana na jana walionekana katika mitaa mbalimbali za Dar es Salaam wakiendelea na mitikasi yao.

Wachezaji ambao waliondoka kwenye kambi hiyo juzi ni Joseph Kaniki, Haruna Moshi ‘Boban’, Mussa Hassan Mgosi, Soud Abdallah,Nurdin Bakar na Moses Odhiambo wakati Akilimali Yahya bado hajapona.