Friday, December 7, 2007

Simba eti nayo 'Uwanjaless' from 1936?


Ndio mnataka kuwa mabingwa wa Afrika hata uwanja hamna? Dalali are you siriazi? Simba bado inahaha kutafuta uwanja wa kufanyia mazoezi baada ya, ule wa Tanganyika Peckers kutumiwa na timu ya Taifa ya Wanawake 'Twiga Star'.


Simba ilikuwa ikitumia uwanja wa Tanganyika Peckers uliopo Kawe jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Zanzibar katika mechi za kujipima nguvu ambapo waliporejea walikuta Twiga wameshawarithi.

msafara wa JK wapata ajali



MSAFARA wa Rais Jakaya Kikwete umepata ajali Wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Ajali hiyo ilitokea jana na kuhusisha magari matatu yalikuwa kwenye msafara huo.

Katibu Tawala Msaidizi mkoani Pwani, Yusuph Matumbo alisema katika jali hiyo hakuna aliyejeruhiwa vibaya bali wengi waliokuwemo ndani ya magari hayo walipata mshituko tu uliosbabisha kupata maumivu ya kichwa.

Jiandaeni kupambana na wanaume akyanani!

MUNGU mkubwa ! habari ndio hiyo kwamba pasipo yeye hakuna kitokacho wala Mzee wa Kutibua asingeweza kuvuma chini ya hili Jua la Bongo ambalo ni 'ova balaa'.
Ndiyo ukweli ulivyo kwamba mambo yamechengi na kimechafuka ndani ya ardhi ya wabongo ndio maana washirika fulani wa Mzee wa Kutibua wameanza kurejea maisha ya bushi.
Lakini mambo ya Mzee wa Kutibua yapo kwenye mpango sahihi na maisha yanasonga kwenye mpango sahihi.
Wala usione soo ndio ishu zenyewe kwamba kuna wakati wa kutembea na kukimbia hata kulia na kucheka ndio maana si ajabu kuona wenye suti zao huko katikati ya Jiji wakigombea Magobore ya kuelekea Shamba.
Au wajanja ambao mida kama hii wamejimwaga kwenye viwanja vyao vya kutumia wakitamba kwamba Noeli ndio imepamba moto huku wengine wakisugua lami huko Samora kuhakikisha kwamba mambo yanakuwa mambo kabla hakijaharibika .
Lakini ikiachwa hiyo ishu, mlichokuwa mkikisubiri kwa hamu ndio hicho sasa kazi kwenu. Ngoma uwanjani mpaka kieleweke Mwekundu wa Msimbazi kivyake na Wanjano Jangwani kinyake.

Simba imepangwa kukipiga kwenye klabu bingwa na Awassa ya Ethiopia na Yanga wanatifuatana na mwakilishi wa Chad au Al Akhdar ya Libya kwenye raundi ya pili ya kombe la Shirikisho kwa vile mwakani iliishia kwenye raundi ya tatu ya Mabingwa na Shirikisho.

Kipute hicho nguo kuchanika, kinaanza mapeema Februari mwakani huku timu nyingi maarufu zikiwa zimefuzu kuziwakilisha nchi zao safari hii hiyo ikimaanisha kuwa patakuwa hapatoshi kama wanavyopenda kutia msisitizo vijana wa tawni.

Simba na Yanga na zenyewe tayari zimeanza maandalizi ya hapa na pale lakini bado hayajafikia kiwango cha kutupa matumaini ya kuona mabadiliko katika michuano ya kimataifa mwaka huu na wala zisitegemee kwamba mwezi Februani ni mbali.

Simba ambayo imekuwa na rekodi ya kuridhisha kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa, yenyewe hata haijaingia kambini na tumekuwa tukishuhudia ikifanya mazoezi yake kwenye uwanja wa Tanganyika Parkers jijini Dar es Salaam na kucheza mechi za kirafiki.

Hatukatai kwamba mechi hizo nazo ni muhimu haswa kwa kujenga timu lakini zisiwadanganye, viongozi na hata makocha wanapaswa kutambua kwamba kambi ni muhimu zaidi si tu kwa ajili ya kuwapa maarifa zaidi wachezaji bali kutambua kiundani hali halisi ya kila mchezaji na kuijenga timu kiufundi zaidi.

Na huwezi ukajiridhisha kwamba una timu nzuri kwa kuangalia majina uliyosajili, ingiza timu kambini uisuke. Hao wachezaji wapya walioongezwa wanapaswa kuwekwa pamoja wenzao, hata Arsenal, Chelsea, Manchester United, Liverpool zenye mastaa kibao zinaheshimu sana suala la kambi.

Huwezi kuweka kambi ya wiki mbili au tatu na kutegemea kufanya vizuri na kuwa na kikosi makini kama mshindani wako au klabu zingine zinazoshiriki michuano hiyo ambazo sasa zipo kambini baadhi ndani ya nchi zao na nyingine nje.

Tuepukane na tabia ya kulipua mambo au kusingizia njaa ya pesa, klabu kubwa kama Simba ikiwa na mazingira mazuri ya kiutendaji na watu makini wanaojali haiwezi kukosa wadhamini watakaomwaga mapesa yatakayoiwezesha kujiendesha kisasa zaidi.

Vurugu za kila leo baina ya viongozi ambazo husababisha kutoelewana ndizo zimekuwa zikiwakatisha tamaa wenye pesa zao kuja kuwekeza kwa vile wanahisi zitatumbuliwa na wajanja wachache au ndio zinaweza zikakuza mgogoro mwingine ambao hauna manufaa kwao.

Simba au Yanga ni klabu kubwa nchini ambazo matajiri wenye biashara zao wanataka kujiingiza ili kuhakikisha kwamba mambo yao yanakwenda sawa lakini mazingira yanakuwa kikwazo na sijui kwanini viongozi waliowekwa madarakani kwa dhamana ya wanachama hawakai wakalitambua hilo.

Kwa jina tu la Simba lilivyo ndani ya nchi haiwezekani ikawa haina hata basi la wachezaji, wachezaji wanapanda daladala wanakwenda mazoezini halafu baada watoke waanza kugombania daladala za kuning’inia karne hii? Na Mishahara yao walipeni kwa wakati pia waishi maisha bora..! alaa.

Tujaribu kubadilika na kujiendesha kisasa zaidi tufike waliko wenzetu, huwezi kuwa kwenye kipindi kigumu kama hiki cha kuelekea kwanza kwenye michuano ya kombe la Kagame Januari halafu Februari klabu Bingwa Afrika unampigisha mchezaji zoezi Kawe halafu jioni unamuachia akarande uswahili. Mnataka kutuitia aibu au?

Mnaweza kusema ni jukumu la kila mchezaji kujichunga lakini mchezaji unayemfanyisha zoezi una uhakika gani kwamba baada ya kuachana na wewe(Kocha, Kiongozi au Daktari) anakwenda kupumzika? Kama anautwika na mpaka usiku wa manane je?

Hatusemi kana kwamba hatuna mifano halisia, tunaona kila siku huku uswahili ! Ndio timu ambayo tunategemea itwae ubingwa wa Afrika? Cheameni Dalali upo hapo? Mnachofanya sasa ni kama kucheza kwenye mdomo wa Mamba mwenye njaa, nini unachotegemea?

Hata Yanga ambayo tayari ipo kambini jijini Mwanza chini ya Kocha wa kizungu, Condic Dusan inapaswa kuwa makini zaidi na kuhakikisha kwamba inawatengenezea wachezaji mazingira mazuri ambayo yatawafanya waelewe kirahisi wanayofungwa na mzungu.

Kuingiza timu kambini haitoshi watu watekelezewe matakwa yao muhimu zaidi ikiwa ni maslahi yao, huyo kocha hawezi kufanikiwa hata kama ana mbinu zinazozidi za Alex Ferguson wa Machester au Arsenal Wenger wa Arsenal endapo atakuwa anafundisha watu wenye matatizo na kulazimika kuuchuna kutokana na nidhamu ya woga.

Makocha hao wanaodaiwa kulipwa mamilioni ya shilingi za kitanzania watafanikiwa endapo kutakuwa na mazingira mazuri ya kazi kubwa ikiwa ni hilo la wachezaji kutengenezewa maisha bora.

Yanga na Simba zinatakiwa kuacha masihara hii ni soka wala siyo biashara ya nazi? Halafu kila mmoja anapaswa kutafuta mechi nzuri za kujipima nguvu ili uonekane udhaifu uko wapi! Huu si wakati wa mazoezi ya mbembwe au mechi za kufurahisha mashabiki. Mtaaibika.

Hii ndio nafasi pekee ya kuthibitisha ukongwe wenu ndani ya Tanzania hata Afrika nzima iwatambue na viongozi wajaribu kuwajenga mashabiki wao wawe na nidhamu na uzalendo.

Mambo ya Simba ikicheza Yanga inazomea au Yanga inacheza Simba inazomea, kuhujumu na kushangilia wageni ni mambo yamepitwa na wakati tupeane changamoto ya ukweli, tupige hatua tutoke kwenye enzi za ushabiki wa kishamba tulionao.

Tupingane, tugombee wachezaji, tuchekane nje ya eneo la uwanja lakini inapofika ndani ya uwanja tubadilike tuige tabia za wenzetu kwenye klabu za Afrika ya Kati. Turingiane mitaani kwa rekodi si kuhujumiana hii ni karne mpya.

Ebwana...eeh. Ni hayo tu! 0714878817
mzeewakutibua.blogspot.com

Nilijua ningeshinda ingawa fitna zilikuwepo!


Rais wa TFF, Leodgar Tenga ambae ameshinda Urais wa CECAFA akisisitiza jambo jijini Dar es Salaam kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Thursday, December 6, 2007

Langa Vipi wewe......!


Umekula pozi kali sana mwana. Kula tano, sasa ina maana hata ukiwa skuli huwezi kutupa dude moja tukaendelea kuburudika nalo wanao? au ndio ushakuwa matawi.

Jamani jamaa wanatuibia kichizi


Msanii wa Bongofleva Q-Chilla akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hapo katikati ya Jiji la Bongo, jamaa anadai Wakenya wanawaibia kichizi nyimbo zao na kuuza kama Ringtone.

Sunday, December 2, 2007

Maximo kwa hili hapa!!!!!!!



WIKIENDI ndio hiyo inajikata na mambo yake kibao ambayo ni mswano zaidi kwa wana wa Dasilamu ambao kwao hakuna linalokatiza bila kutestiwa sambamba na matanuzi kama kawa.
Ambao wameshaseti mambo yao wanatamani hata huyo Mkuu wa Kaya, angetangaza evuridei ni wikiendi tu ingawa wapo wanaolaani mambo yanavyokwenda kwa vile hali si hali.
Wanatamani hata kurudisha laifu ya enzi hizo kileji lakini ah wapi. Soli zinazidi kutoboka kutokana na mapambano na lami za kisasa walizotuwekea mpaka uswahili hao mnaowaita Tanrodi.
Washirika wako kwenye hesabu kali, kutafakari jinsi ya kufunga mambo na viwalo vya klithmasi. Unafanya mchezo nini ndio bongo hiyo?
Usione wenye suti zao wanamwagika jasho ukadhani ni msongamano wa kwenye daladala za Mwenge- Posta. Wenzio wamepiga mguu kutoka Posta Mpya mpaka Mwananyamala kwa Manjunju.
We hujasikia wenzio wanakuambia Mjini Shule ndio mambo hayo ya kiutu uzima, kinaeleweka kwa vyovyote vile hata kwa kusaga lami nani arudi kijiji kwenye vibatari wakati mishumaa ipo hata msikiti wa jirani au Chachi itaibwa Tanesco wakikwapua umeme wao.
Unafikiri wote wenye vitambi huko Dasilamu mjini ndio wala vyuku na bia huko Kempski? Wengine mambo ya Wali Maharage tu wa jero na maji ya fifte kwa Kariakoo tu.
Ndio tawni hiyo bro akili kichwani. Lakini nimeskia na jamaa yenu naye kaanza, akifanikiwa kuwarudisha tena Brazil safari hii atashindwaje kuwaambia kazaliwa Kishumundu?
Ameanza tena! hajui hata kama wengine tukikumbuka machungu ya kipigo cha 4-0 tulichokula Senegal miezi fulani iliyopita tukachanganyikiwa.
Lakini wiki hii baada tu ya kuiona ratiba ya kufuzu Sauzi kwenye kombe la Dunia 2010, yule yule Marcio Maximo kocha wetu huyo! Wa Stars ameanza hadithi za kambi ya Brazil.
Hivi kuna nini? Halafu anashikilia bango kana kwamba ndio kila kitu kipo huko na tusipokwenda tumekwisha. Ndio tunaheshimu kwamba angalau ameleta changamoto kwa wachezaji na mashabiki tangu aanze kufanya mambo Stars miezi kadhaa iliyopita, lakini kwa hili mimi hapana! No. Amekuwa akisisitiza wiki hii kwamba lazima airejeshe Stars mwakani, Brazili alikokuwa ameweka kambi kabla ya kuvaa na Senegal jijini Dakar.
Sababu zake ni kwamba anataka kwenda kumalizia programu aliyoianza Januari alipopiga kambi ya mwezi mmoja, tukapigwa fiksi kwamba tumetisha, wote hao Botafogo,Fluminence, Flamingo na Vasco da Gama wanatupigia saluti vibaya sana kutokana na kiwango.
Vasco da Gama, ambayo iliifunga Manchesta (hiyo ya Fagasoni) 3-0 eti Stars iliitesa mpaka ikaomba mpira uishe eti! jamani mtatudanganya mpaka lini?
Wanaofanya kazi kama ya Mzee wa Kutibua wakatuandikia 'makala za kufa mtu' kwamba Stars Kiboko, tishio Brazil, makocha wameivulia kofia na wengine wakathubutu kwenda mbaa...li eti na wachezaji wetu kina nanihii na wenyewe wamekuwa lulu wanasakwa kila kona.
Wamekuwa juu eti hata kuliko Wabrazil wenyewe ambao kila leo wanamwagika Ulaya, sembuse sisi ambao hata Uarabuni tunanyatia kuingia tena tukienda tunatisha kwenye mabonanza ya Machimbo?
Kimsingi sikubaliani hata kidogo na hoja za Maximo kuhusiana na uamuzi wake wa kupeleka timu Brazil kwa mara nyingine, wala sidhani kwamba kuna ulazima wa anachotaka kutushawishi tumuelewa, labda atumie nguvu nyingine sababu hata Tiefuefu yenyewe ambayo ndio inayopaswa kuratibu ishu kama hizo haijasikika ikichangia lolote kuhusiana na safari hiyo kitu ambacho kinanipa wasiwasi.
Yawezekana Maximo ana malengo, lakini si kwa uchumi wa Tanzania hii ya sasa. Januari alikuwa na kikosi cha Wanaume kama 25 ambao kwa makadirio ya haraka alitumia mil. 100 za wadhamini Brazil ambako baadaye tukafungwa na Senegal akapukutisha karibu nusu na kuita wapya.
Sasa hata kama ni programu ya muda mrefu ameandaa mbona wale aliokwenda nao mwanzoni amewapukutisha kiasi hicho na hata waliko hatuwasikii tena hata wanachofanya na kama atawaita tena kwa faida ya nani?
Muendelezo utatoka wapi wakati kikosi kilichopo kambini kina wachezaji kibao wapya, ina maana atakwenda kukaa miezi miwili tena aanze moja? mbona anatupa maswali magumu, au kuna kitu anatafuta Brazili?
Hata kama lengo lake ni kurejesha wale wa mwanzo akaendelee nao kwanini aliwaacha halafu sasa awaone lulu? Katika mkutano na waandishi alikiri amefanya mazungumzo na wadhamini kuhusiana na hilo. Hivi nini kazi ya Tiefuefu na maofisa wake kama mpaka Kocha ana nguvu ya kupita mpaka kupeleka muhtasari wake kwa mdhamini bila kuwahusisha?
Kwanini Maximo asiweke kambi ya muda mfupi kwenye nchi zenye kiwango cha juu Afrika na kucheza mechi kadhaa za kirafiki na timu imara kuliko kwenda kucheza mabonanza Brazil na klabu ambazo siamini zinaweza kutusaidia lolote hata tukikaa miezi sita!
Yatakuwa ni yale yale ya kucheza na timu C mwisho wa siku tunavimba vifua kwamba tunajua na kuunguza manoti kumbe wapi. Nchi za Afrika kwa mfano, Misri, Tunisia, Sudan,Ghana, Angola tukizitumia zinaweza kutujenga zaidi kuliko kukimbilia Brazil hata tukicheza na klabu kama Zamalek, Al-ahly, Al-Merrekh zinaweza kutusaidia kuliko kwenda kufanya mazoezi kwenye viwanja vya Brazil, naanza pengine kupata hata wasiwasi na washauri wa Maximo na uhusiano wake kimaamuzi na Tiefuefu ya Leodgar Tenga.
Isifike mahali wadhamini pia wakatuendesha wanavyotaka lazima Tiefuefu iwe na maamuzi na kuangalia hadhi ya timu ya Taifa na sababu za msingi za kila inapokanyaga timu hiyo, ni mali ya Watanzania hiyo si klabu ya wanachama 300 wanaoweza kukutana Msimbazi wakamng'oa Dalali au Jangwani wakamtosa Madega.
Lazima kuangalia faida, hasara mwisho wa siku nyie ndio mnaonekana hovyo, au tubaki kuamini kwamba Maximo anawaendesha kama tunavyosikia huku mtaani?