Friday, December 7, 2007

Simba eti nayo 'Uwanjaless' from 1936?


Ndio mnataka kuwa mabingwa wa Afrika hata uwanja hamna? Dalali are you siriazi? Simba bado inahaha kutafuta uwanja wa kufanyia mazoezi baada ya, ule wa Tanganyika Peckers kutumiwa na timu ya Taifa ya Wanawake 'Twiga Star'.


Simba ilikuwa ikitumia uwanja wa Tanganyika Peckers uliopo Kawe jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Zanzibar katika mechi za kujipima nguvu ambapo waliporejea walikuta Twiga wameshawarithi.

msafara wa JK wapata ajali



MSAFARA wa Rais Jakaya Kikwete umepata ajali Wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Ajali hiyo ilitokea jana na kuhusisha magari matatu yalikuwa kwenye msafara huo.

Katibu Tawala Msaidizi mkoani Pwani, Yusuph Matumbo alisema katika jali hiyo hakuna aliyejeruhiwa vibaya bali wengi waliokuwemo ndani ya magari hayo walipata mshituko tu uliosbabisha kupata maumivu ya kichwa.

Jiandaeni kupambana na wanaume akyanani!

MUNGU mkubwa ! habari ndio hiyo kwamba pasipo yeye hakuna kitokacho wala Mzee wa Kutibua asingeweza kuvuma chini ya hili Jua la Bongo ambalo ni 'ova balaa'.
Ndiyo ukweli ulivyo kwamba mambo yamechengi na kimechafuka ndani ya ardhi ya wabongo ndio maana washirika fulani wa Mzee wa Kutibua wameanza kurejea maisha ya bushi.
Lakini mambo ya Mzee wa Kutibua yapo kwenye mpango sahihi na maisha yanasonga kwenye mpango sahihi.
Wala usione soo ndio ishu zenyewe kwamba kuna wakati wa kutembea na kukimbia hata kulia na kucheka ndio maana si ajabu kuona wenye suti zao huko katikati ya Jiji wakigombea Magobore ya kuelekea Shamba.
Au wajanja ambao mida kama hii wamejimwaga kwenye viwanja vyao vya kutumia wakitamba kwamba Noeli ndio imepamba moto huku wengine wakisugua lami huko Samora kuhakikisha kwamba mambo yanakuwa mambo kabla hakijaharibika .
Lakini ikiachwa hiyo ishu, mlichokuwa mkikisubiri kwa hamu ndio hicho sasa kazi kwenu. Ngoma uwanjani mpaka kieleweke Mwekundu wa Msimbazi kivyake na Wanjano Jangwani kinyake.

Simba imepangwa kukipiga kwenye klabu bingwa na Awassa ya Ethiopia na Yanga wanatifuatana na mwakilishi wa Chad au Al Akhdar ya Libya kwenye raundi ya pili ya kombe la Shirikisho kwa vile mwakani iliishia kwenye raundi ya tatu ya Mabingwa na Shirikisho.

Kipute hicho nguo kuchanika, kinaanza mapeema Februari mwakani huku timu nyingi maarufu zikiwa zimefuzu kuziwakilisha nchi zao safari hii hiyo ikimaanisha kuwa patakuwa hapatoshi kama wanavyopenda kutia msisitizo vijana wa tawni.

Simba na Yanga na zenyewe tayari zimeanza maandalizi ya hapa na pale lakini bado hayajafikia kiwango cha kutupa matumaini ya kuona mabadiliko katika michuano ya kimataifa mwaka huu na wala zisitegemee kwamba mwezi Februani ni mbali.

Simba ambayo imekuwa na rekodi ya kuridhisha kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa, yenyewe hata haijaingia kambini na tumekuwa tukishuhudia ikifanya mazoezi yake kwenye uwanja wa Tanganyika Parkers jijini Dar es Salaam na kucheza mechi za kirafiki.

Hatukatai kwamba mechi hizo nazo ni muhimu haswa kwa kujenga timu lakini zisiwadanganye, viongozi na hata makocha wanapaswa kutambua kwamba kambi ni muhimu zaidi si tu kwa ajili ya kuwapa maarifa zaidi wachezaji bali kutambua kiundani hali halisi ya kila mchezaji na kuijenga timu kiufundi zaidi.

Na huwezi ukajiridhisha kwamba una timu nzuri kwa kuangalia majina uliyosajili, ingiza timu kambini uisuke. Hao wachezaji wapya walioongezwa wanapaswa kuwekwa pamoja wenzao, hata Arsenal, Chelsea, Manchester United, Liverpool zenye mastaa kibao zinaheshimu sana suala la kambi.

Huwezi kuweka kambi ya wiki mbili au tatu na kutegemea kufanya vizuri na kuwa na kikosi makini kama mshindani wako au klabu zingine zinazoshiriki michuano hiyo ambazo sasa zipo kambini baadhi ndani ya nchi zao na nyingine nje.

Tuepukane na tabia ya kulipua mambo au kusingizia njaa ya pesa, klabu kubwa kama Simba ikiwa na mazingira mazuri ya kiutendaji na watu makini wanaojali haiwezi kukosa wadhamini watakaomwaga mapesa yatakayoiwezesha kujiendesha kisasa zaidi.

Vurugu za kila leo baina ya viongozi ambazo husababisha kutoelewana ndizo zimekuwa zikiwakatisha tamaa wenye pesa zao kuja kuwekeza kwa vile wanahisi zitatumbuliwa na wajanja wachache au ndio zinaweza zikakuza mgogoro mwingine ambao hauna manufaa kwao.

Simba au Yanga ni klabu kubwa nchini ambazo matajiri wenye biashara zao wanataka kujiingiza ili kuhakikisha kwamba mambo yao yanakwenda sawa lakini mazingira yanakuwa kikwazo na sijui kwanini viongozi waliowekwa madarakani kwa dhamana ya wanachama hawakai wakalitambua hilo.

Kwa jina tu la Simba lilivyo ndani ya nchi haiwezekani ikawa haina hata basi la wachezaji, wachezaji wanapanda daladala wanakwenda mazoezini halafu baada watoke waanza kugombania daladala za kuning’inia karne hii? Na Mishahara yao walipeni kwa wakati pia waishi maisha bora..! alaa.

Tujaribu kubadilika na kujiendesha kisasa zaidi tufike waliko wenzetu, huwezi kuwa kwenye kipindi kigumu kama hiki cha kuelekea kwanza kwenye michuano ya kombe la Kagame Januari halafu Februari klabu Bingwa Afrika unampigisha mchezaji zoezi Kawe halafu jioni unamuachia akarande uswahili. Mnataka kutuitia aibu au?

Mnaweza kusema ni jukumu la kila mchezaji kujichunga lakini mchezaji unayemfanyisha zoezi una uhakika gani kwamba baada ya kuachana na wewe(Kocha, Kiongozi au Daktari) anakwenda kupumzika? Kama anautwika na mpaka usiku wa manane je?

Hatusemi kana kwamba hatuna mifano halisia, tunaona kila siku huku uswahili ! Ndio timu ambayo tunategemea itwae ubingwa wa Afrika? Cheameni Dalali upo hapo? Mnachofanya sasa ni kama kucheza kwenye mdomo wa Mamba mwenye njaa, nini unachotegemea?

Hata Yanga ambayo tayari ipo kambini jijini Mwanza chini ya Kocha wa kizungu, Condic Dusan inapaswa kuwa makini zaidi na kuhakikisha kwamba inawatengenezea wachezaji mazingira mazuri ambayo yatawafanya waelewe kirahisi wanayofungwa na mzungu.

Kuingiza timu kambini haitoshi watu watekelezewe matakwa yao muhimu zaidi ikiwa ni maslahi yao, huyo kocha hawezi kufanikiwa hata kama ana mbinu zinazozidi za Alex Ferguson wa Machester au Arsenal Wenger wa Arsenal endapo atakuwa anafundisha watu wenye matatizo na kulazimika kuuchuna kutokana na nidhamu ya woga.

Makocha hao wanaodaiwa kulipwa mamilioni ya shilingi za kitanzania watafanikiwa endapo kutakuwa na mazingira mazuri ya kazi kubwa ikiwa ni hilo la wachezaji kutengenezewa maisha bora.

Yanga na Simba zinatakiwa kuacha masihara hii ni soka wala siyo biashara ya nazi? Halafu kila mmoja anapaswa kutafuta mechi nzuri za kujipima nguvu ili uonekane udhaifu uko wapi! Huu si wakati wa mazoezi ya mbembwe au mechi za kufurahisha mashabiki. Mtaaibika.

Hii ndio nafasi pekee ya kuthibitisha ukongwe wenu ndani ya Tanzania hata Afrika nzima iwatambue na viongozi wajaribu kuwajenga mashabiki wao wawe na nidhamu na uzalendo.

Mambo ya Simba ikicheza Yanga inazomea au Yanga inacheza Simba inazomea, kuhujumu na kushangilia wageni ni mambo yamepitwa na wakati tupeane changamoto ya ukweli, tupige hatua tutoke kwenye enzi za ushabiki wa kishamba tulionao.

Tupingane, tugombee wachezaji, tuchekane nje ya eneo la uwanja lakini inapofika ndani ya uwanja tubadilike tuige tabia za wenzetu kwenye klabu za Afrika ya Kati. Turingiane mitaani kwa rekodi si kuhujumiana hii ni karne mpya.

Ebwana...eeh. Ni hayo tu! 0714878817
mzeewakutibua.blogspot.com

Nilijua ningeshinda ingawa fitna zilikuwepo!


Rais wa TFF, Leodgar Tenga ambae ameshinda Urais wa CECAFA akisisitiza jambo jijini Dar es Salaam kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Thursday, December 6, 2007

Langa Vipi wewe......!


Umekula pozi kali sana mwana. Kula tano, sasa ina maana hata ukiwa skuli huwezi kutupa dude moja tukaendelea kuburudika nalo wanao? au ndio ushakuwa matawi.

Jamani jamaa wanatuibia kichizi


Msanii wa Bongofleva Q-Chilla akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hapo katikati ya Jiji la Bongo, jamaa anadai Wakenya wanawaibia kichizi nyimbo zao na kuuza kama Ringtone.

Sunday, December 2, 2007

Maximo kwa hili hapa!!!!!!!



WIKIENDI ndio hiyo inajikata na mambo yake kibao ambayo ni mswano zaidi kwa wana wa Dasilamu ambao kwao hakuna linalokatiza bila kutestiwa sambamba na matanuzi kama kawa.
Ambao wameshaseti mambo yao wanatamani hata huyo Mkuu wa Kaya, angetangaza evuridei ni wikiendi tu ingawa wapo wanaolaani mambo yanavyokwenda kwa vile hali si hali.
Wanatamani hata kurudisha laifu ya enzi hizo kileji lakini ah wapi. Soli zinazidi kutoboka kutokana na mapambano na lami za kisasa walizotuwekea mpaka uswahili hao mnaowaita Tanrodi.
Washirika wako kwenye hesabu kali, kutafakari jinsi ya kufunga mambo na viwalo vya klithmasi. Unafanya mchezo nini ndio bongo hiyo?
Usione wenye suti zao wanamwagika jasho ukadhani ni msongamano wa kwenye daladala za Mwenge- Posta. Wenzio wamepiga mguu kutoka Posta Mpya mpaka Mwananyamala kwa Manjunju.
We hujasikia wenzio wanakuambia Mjini Shule ndio mambo hayo ya kiutu uzima, kinaeleweka kwa vyovyote vile hata kwa kusaga lami nani arudi kijiji kwenye vibatari wakati mishumaa ipo hata msikiti wa jirani au Chachi itaibwa Tanesco wakikwapua umeme wao.
Unafikiri wote wenye vitambi huko Dasilamu mjini ndio wala vyuku na bia huko Kempski? Wengine mambo ya Wali Maharage tu wa jero na maji ya fifte kwa Kariakoo tu.
Ndio tawni hiyo bro akili kichwani. Lakini nimeskia na jamaa yenu naye kaanza, akifanikiwa kuwarudisha tena Brazil safari hii atashindwaje kuwaambia kazaliwa Kishumundu?
Ameanza tena! hajui hata kama wengine tukikumbuka machungu ya kipigo cha 4-0 tulichokula Senegal miezi fulani iliyopita tukachanganyikiwa.
Lakini wiki hii baada tu ya kuiona ratiba ya kufuzu Sauzi kwenye kombe la Dunia 2010, yule yule Marcio Maximo kocha wetu huyo! Wa Stars ameanza hadithi za kambi ya Brazil.
Hivi kuna nini? Halafu anashikilia bango kana kwamba ndio kila kitu kipo huko na tusipokwenda tumekwisha. Ndio tunaheshimu kwamba angalau ameleta changamoto kwa wachezaji na mashabiki tangu aanze kufanya mambo Stars miezi kadhaa iliyopita, lakini kwa hili mimi hapana! No. Amekuwa akisisitiza wiki hii kwamba lazima airejeshe Stars mwakani, Brazili alikokuwa ameweka kambi kabla ya kuvaa na Senegal jijini Dakar.
Sababu zake ni kwamba anataka kwenda kumalizia programu aliyoianza Januari alipopiga kambi ya mwezi mmoja, tukapigwa fiksi kwamba tumetisha, wote hao Botafogo,Fluminence, Flamingo na Vasco da Gama wanatupigia saluti vibaya sana kutokana na kiwango.
Vasco da Gama, ambayo iliifunga Manchesta (hiyo ya Fagasoni) 3-0 eti Stars iliitesa mpaka ikaomba mpira uishe eti! jamani mtatudanganya mpaka lini?
Wanaofanya kazi kama ya Mzee wa Kutibua wakatuandikia 'makala za kufa mtu' kwamba Stars Kiboko, tishio Brazil, makocha wameivulia kofia na wengine wakathubutu kwenda mbaa...li eti na wachezaji wetu kina nanihii na wenyewe wamekuwa lulu wanasakwa kila kona.
Wamekuwa juu eti hata kuliko Wabrazil wenyewe ambao kila leo wanamwagika Ulaya, sembuse sisi ambao hata Uarabuni tunanyatia kuingia tena tukienda tunatisha kwenye mabonanza ya Machimbo?
Kimsingi sikubaliani hata kidogo na hoja za Maximo kuhusiana na uamuzi wake wa kupeleka timu Brazil kwa mara nyingine, wala sidhani kwamba kuna ulazima wa anachotaka kutushawishi tumuelewa, labda atumie nguvu nyingine sababu hata Tiefuefu yenyewe ambayo ndio inayopaswa kuratibu ishu kama hizo haijasikika ikichangia lolote kuhusiana na safari hiyo kitu ambacho kinanipa wasiwasi.
Yawezekana Maximo ana malengo, lakini si kwa uchumi wa Tanzania hii ya sasa. Januari alikuwa na kikosi cha Wanaume kama 25 ambao kwa makadirio ya haraka alitumia mil. 100 za wadhamini Brazil ambako baadaye tukafungwa na Senegal akapukutisha karibu nusu na kuita wapya.
Sasa hata kama ni programu ya muda mrefu ameandaa mbona wale aliokwenda nao mwanzoni amewapukutisha kiasi hicho na hata waliko hatuwasikii tena hata wanachofanya na kama atawaita tena kwa faida ya nani?
Muendelezo utatoka wapi wakati kikosi kilichopo kambini kina wachezaji kibao wapya, ina maana atakwenda kukaa miezi miwili tena aanze moja? mbona anatupa maswali magumu, au kuna kitu anatafuta Brazili?
Hata kama lengo lake ni kurejesha wale wa mwanzo akaendelee nao kwanini aliwaacha halafu sasa awaone lulu? Katika mkutano na waandishi alikiri amefanya mazungumzo na wadhamini kuhusiana na hilo. Hivi nini kazi ya Tiefuefu na maofisa wake kama mpaka Kocha ana nguvu ya kupita mpaka kupeleka muhtasari wake kwa mdhamini bila kuwahusisha?
Kwanini Maximo asiweke kambi ya muda mfupi kwenye nchi zenye kiwango cha juu Afrika na kucheza mechi kadhaa za kirafiki na timu imara kuliko kwenda kucheza mabonanza Brazil na klabu ambazo siamini zinaweza kutusaidia lolote hata tukikaa miezi sita!
Yatakuwa ni yale yale ya kucheza na timu C mwisho wa siku tunavimba vifua kwamba tunajua na kuunguza manoti kumbe wapi. Nchi za Afrika kwa mfano, Misri, Tunisia, Sudan,Ghana, Angola tukizitumia zinaweza kutujenga zaidi kuliko kukimbilia Brazil hata tukicheza na klabu kama Zamalek, Al-ahly, Al-Merrekh zinaweza kutusaidia kuliko kwenda kufanya mazoezi kwenye viwanja vya Brazil, naanza pengine kupata hata wasiwasi na washauri wa Maximo na uhusiano wake kimaamuzi na Tiefuefu ya Leodgar Tenga.
Isifike mahali wadhamini pia wakatuendesha wanavyotaka lazima Tiefuefu iwe na maamuzi na kuangalia hadhi ya timu ya Taifa na sababu za msingi za kila inapokanyaga timu hiyo, ni mali ya Watanzania hiyo si klabu ya wanachama 300 wanaoweza kukutana Msimbazi wakamng'oa Dalali au Jangwani wakamtosa Madega.
Lazima kuangalia faida, hasara mwisho wa siku nyie ndio mnaonekana hovyo, au tubaki kuamini kwamba Maximo anawaendesha kama tunavyosikia huku mtaani?

Friday, November 30, 2007

Angetile naye alikuwepo


Mmoja wa washirika wa Mzee wa Kutibua Angetile Osiah(anayeanguka) akishindwa kuhimili vishindo kwenye tamasha la Waandishi lililofanyika hapo Dar

Monday, November 26, 2007

Ayaa..! Anaanguka hata boli haijafika


Kipa wa timu ya Wanawake wa Zanzibar, Zanzibar Heroes iliyopigwa bao 17-0 na Twiga Stars kwenye uwanja wa Taifa wa zamani wenye nyasi bandia. Hawa mademu walikiona cha moto, eti kocha anadai uwanja umewazingua eti halafu walilala kwenye jahazi.

Nyie ni watu muhimu sana ingawa mlikuwa mnaniua mida fulani


Nahodha mstaafu wa Taifa Stars, Mecky Maxime akiaga waandishi wa michezo katika mechi maalum ya kumuaga iliyoandaliwa na TFF siku fulani zilizopita. Jamaa alifunika kinoma, haijapata kutokea Bongo

Friday, November 23, 2007

"Leaders of conflict and gate collection"

WASHIKAJI mambo vipi hapo! Mwanenu nipo freshi kimtindo ingawa bongo kimechafuka kinoma wanangu. Joto kichizi wenye ngozi za vyura tu ndio wanaopeta.

Sijui ndio kiama chenyewe kinaanza kubipu bipu kiaina maana wenye jiji letu hatuelewi elewi jinsi ngoma inavyovuma kila panapoguswa hali si shwari.

Ingawa mambo fulani ni shwari wanangu wa Lugalo soo soo.. kabisa! Sijui ni ushamba au labda kwa vile ni mara kwanza kuwaibukia ebu tuwachukulie ndio fasheni.

Ngoja sasa nikupe ishu yenyewe! Mzee mzima kama kawa mambo ya kujirusha mitaa ya Bongo wikiendi siunajua ndio zake? Sasa wikiendi hiyo iliyopita masela kama saba hivi wenye nyadhifa zao wamejimwaga naiti klabu moja hapa mitaa ya Lugalo kama unaenda Tegeta. Wenyewe siku hizi wanaita Bondeni.

Wadau wakamuendea hewani Mzee mzima nikaibuka eneo la tukio tayari kushusha kitu sehemu fulani huku ukihudumiwa kama ‘Presidaa’ kutokana na unyeti wako kwenye eneo la tukio ambalo wamo jamaa wenye minoti yao ya kusumbua tawni fulu taimu.

Kuna makelele mengi humu ndani lakini baadae jinsi muda unavyokwenda unakuja kugundua kwamba kuna kikundi kingine cha jamaa kama sita kwa nyuma yenu ambao karibu wote ni kutoka kwenye hii jamii ya jamaa fulani(ya kanda ya ziwa wananihii…) ambao wanajifanya Inglishi ni sehemu ya laifu yao toka Kileji.

“Ofukozi Rwego (Rwegoshora) mpe coldi wani, halafu athazi ai don rimemba” ni kauli ya mmoja wa hao jamaa kwenye hiyo meza iliyojaa kina Rwechungura, Kaijage na wengine wengine (nimewasahau).

Baadaye kidogo wameshaanza kuzungukwa zungukwa na viumbe fulani (viburudisho wenyewe wanaviita).Ghafla huko kwenye dansini floo Dijei akaweka “Hapo vipii..” ya huyu mwanabongofleva mnayemuita Profesa nanihii…Jei.

Jamaa wawili wakaibuka zao kwenye dansin floo kuyarudi mangoma, hapo ndipo ishu iliponoga sasa jamaa walikuwa wanakata zao Tusker na Nondo sijui ndio ubrazameni wenyewe jamaa (Rwego) kachomoka kaunta fasta kaibuka chukua zake hiyo nanihii ya chupa ya kijani… Bavaria na ufunguo wa gari kaenda kuyarudi.

“Kinda gateni mpaka chuoni kikuu longi taimu kwa machizi na masista duu…” ndivyo anavyokwenda sambamba na vesi za huo mziki, huku akiwa katikati kabisa ya masela kibao(hiyo ni naiti kali). Wanaomfahamu wanapigwa butwaa kwa jinsi anavyonyanyua juu Bavaria na ufunguo wa gari hawaelewi elewi. Wengine wanafikiri labda kashinda kwenye promosheni hapo nje dakika kadhaa zilizopita ndio anasherekea.
Lakini jamaa zake wanaoendelea na kilaji mezani wanamsanifu tu “Cheki jamaa ayah…! Kashaachana na hii sasa ana Bavaria siumeona mikono ile? Mwingine anayeonekana kumfahamu vilivyo akadakia “Hamna hiyo atakuja kuinywa sianamtaka Eliza pale (ananyooshea kidole meza nyingine) anataka aone kwamba na yeye matawi halafu na usafiri haumpigi chenga”.

Duh! Hivi kumbe bado hizi staili bado zipo? Duh! Ndio matatizo ya kuvamia jiji la watu sasa hata kama umepiga skuli bado wakuja tu.

Lakini wanangu ebu ngoja kidogo tuachane na Rwego tucheki na ishu zingine huko Dasilamu mjini. Nimeskia kuna ‘Maprofesa’ wamemwaga wino tayari kutoa ‘lekcha’ Jangwani.

Huyo bosi nimebonyezwa anaitwa Condic Dusan na msaidizi, Solokoviskiii na naskia wameshapewa rungu na tayari kufanya baadhi ya ishu ili kuhakikisha neksti raundi ya Ligi Kuu kinaeleweka Jangwani. Lakini Wekundu wataachia hilo kopo la ubingwa? Simo!

Kitendo cha Yanga kuleta makocha hao raia wa Serbia ni changamoto kubwa katika soka la Tanzania ambayo inastahili kuigwa na klabu zote za Ligi Kuu ili kuinua kiwango na kubadili taswira ya soka la Bongo.

Kama ilivyo kwa wadau wengine wa Bara, naungana na wadau wengine ambao wamekuwa wakisema kwamba huenda kukawepo na changamoto kubwa kwenye Ligi haswa kutokana na uzoefu, rekodi na utaalam wa makocha hao ambao wametamba na klabu kadhaa maarufu za Afrika ya Kati na Magharibi.
Si suala la kupongezwa tu. Uongozi wa Yanga unapaswa kuacha ubabaishaji nikiwa namaanisha kwamba unapaswa kutoa ushirikiano na sapoti ya kila aina kwa makocha hao.Vinginevyo muda si mrefu watapotea tena kama walivyopotea wengine, wala hakuna atakayeshangaa.

Hao jamaa msiwageuze wadoli kwamba mmewaleta ili kujionyesha kwamba mnaweza au mna jeuri ya fedha haisaidii!

Hii kauli aliyokuwa akipenda kuitumia huyu kocha Mserbia Sredjoviv Milutin ‘Micho’ kwamba Yanga ina baadhi ya viongozi ambao ni “Leaders of Conflict and gate collection (viongozi wa migogoro na mapato ya milangoni)” ndio moja kati ya sababu zilizomfanya akashindwa kufanya mambo yake naamini bado ina ukweli ndani yake.

Sishawishiki kuamini kwamba hali hiyo imekwisha ndani ya Yanga kwa kipindi hiki cha miezi michache tangu Micho ambaye alikuwa amezoea mazingira ya ‘kiswahili’ atimke Jangwani.

Viongozi wenyewe kwa wenyewe wanapaswa kuhakikisha kwamba kila mmoja anawajibika kwa nafasi yake na hata kama ikiwezekana ziwepo kamati ndogondogo za watu makini ambao watapewa majukumu ili kuwarahishia kazi hao makocha wa kigeni.

Kuwa mzungu si kujua kila kitu, na si lazima kila kitu afanye Mwenyekiti au Katibu huu ni wakati wa mgawanyo wa majukumu. Si mtu unakaa Dar es Salaam wiki nzima wala hujui ilipo timu halafu unaskia inacheza Mbeya jumamosi unakwea pipa Ijumaa kwenda kusimamia mapato na baadae unapotea kwenye mazingira ya utatanishi.
Ebwana habari ndio hiyo! Mida basi masela.

Friday, November 2, 2007

Hii ya Nsajigwa na Ivo ni kafara

HEE..! Washikaji ndio Novemba hilo ndani ya nyumba kama masihara vile, wazee wazima ndio tunazidi kwenda eji tu kiutani utani mara unakuwa zilipendwa.

Ndio muda wa mahesabu unakaribia wanangu na mambo ya minuso minuso ya klithmasi araundi ze kona kazi kwenu sasa, ila kazi ipo unaweza kujikuta ukijibinafsisha hivi hivi.

Mambo yako kwenye mstari kiaina kwa Mzee wa Kutibua na angali akidunda uraiani kwa jeuri ingawa jua la Bongo linazingua upara wake. Si unajua aliamua kulikwaruza baada ya vinyweleo vyeupe kuanza kumnyemelea?

Ngoja nikumegeeni kwanza hii! Siku kama nne hivi zilizopita Mzee mzima niliibuka kwenye Kabaa fulani hivi mitaa ya Keinyama hapo, kwa mualiko wa mzito wa mdau fulani wa muziki wa bongo.

Siunajua tena mwanangu sehemu kama hizo, kilaji na mambo fulani fulani si ya kuuliza? Kwenye meza wapo washikadau kama wanne hivi.(ukijiskia waite kwa majina yao ya serikali.. Shekigenda, Babuu, Tesha na huyu wa mwisho nani huyu … Lucas).

Usimhesabie huyo Byarugaba ambaye alianza kutwanga nanihii..Kesto tangu mida ya lanchi alipoenda kwenye Eitimu akakuta Mpunga wa mwezi tayari umeshajaa. Yeye tayari kashazimia kitaambo, kaegemea kiti. Kinachotoka mdomoni ni kauli moja tu “…mmhh!”.

Walioko kwenye meza ya Mzee wa Kutibua ni wazito na jamaa fulani fulani huku pembeni shingo ni nyingi zinahaha kuangalia mchakato unavyokwenda, pengine ni kutokana na mijusi mizito waliyotinga washikadau ambayo kwa kawaida ya kiwanja tulichopo inahesabika au wakati mwingine haipo kabisa.

Ghafla huku nyuma kaibuka jamaa (rapa wa bendi moja hapo kinondoni) wa bendi maarufu ya Bongo kaanza kutoa salamu akiwa mita kama mia hivi “Pedeshee Shekii…, Pedeshee Shekii…” Tesha akasemaa ohooo… “kimechafuka, mtu wa mizinga huyo kashavamia, hakawii kugeuza steji hapa”

Jamaa kama vile kazilalia sana jana anavyoonekana halafu bigi chachaa mifukoni, kabla ya kupiga mzinga dada nanihii ambaye amekulia ng’ambo ya bahari (Mkunazini) kashafika karibu akamhudumia, jamaa si akaanza kuzichapa kwa hasira kama anakomoa!

Kafyonza hizo wanazoita nondo kama nane ivi ndani ya dakika chache, hajui kama kuna mnene aliyemtengea fifte ya kumkomesha, ameanza ya tisa tu hoi ngoma ikaanza kuzomea sakafu.

Ayaah…! Aibu.. watu wote mikono mdomoni wanashangaa, mambo si mambo mtu mzima kashaharibu faragha hakieleweki tena wala hata macho hataki kufungua. Kwa umbaalii anasema eeehh.. eehh! Mwanangu aibuu… watu wamebeba kama nanihii.

Lakini..! Ebu ngoja tuchenji chaneli kwanza, siku siyo nyingi sana Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa wamefungiwa na klabu hiyo miezi sita kutokana na mambo kibaaoo moja wapo likiwa ni madai ya hujuma na utovu wa nidhamu.

Wachezaji hao wanadaiwa kuhujumu timu hiyo ikafungwa na Simba 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Bara wiki sio nyingi zilizopita huko Morogoro na baadae kutoroka kambini bila taarifa kitendo kilichotafsiriwa kama utoro kazini na utovu wa nidhamu.

Wadau wa soka ambao hawafungamani na upande wowote walionyesha kushangazwa na kitendo cha kundi la mashabiki wa Yanga kumvamia na kumpiga vibaya Mapunda baada ya mechi hiyo kwa kile walichodai kuwa aliwafungisha, huku wachezaji kadhaa nao wakiambulia matusi na wengine wakitembea si mita nyingi na Polisi wakutuliza ghasia.

Lakini cha ajabu na ambacho kinashangaza wengi Ivo angeweza hata kufa kwa ajili ya makosa ya kibinadamu ya sekundu moja tu akiwa langoni. Kwanza hakuna kiongozi yoyote wa Yanga aliyeonyesha ubinadamu kwa kuibuka na kumnusuru Ivo alivyokuwa akipambana na mashabiki je? Kama si Polisi waliofanya jitihada za makusudi nini kingetokea kwa kipa huyo wa timu ya Taifa.

Achana na hilo, viongozi hao hao ambao ndio wanaowajibika na usalama wa mchezaji mbali na kwamba hata kambini hakuna aliyefika kumjulia hali kibinadamu baada ya mchezo huo, hakuna pia ambae aliyekuwa akijali hali ya vitisho kwenye simu na mitaani alivyokuwa akipata mchezaji.

Sasa katika mazingira kama hayo, unategemea mchezaji aendelee tu kuendelea kuishi kambini na kuitumikia timu katika mazingira gani wakati hata kocha mwenyewe, ameshanukuliwa na vyombo vya habari akidai kwamba ni kosa la kipa limewanyima ushindi?

Hali hiyo ndio iliyowakumba na wachezaji wengine kama Nsajigwa na Amir Maftah ambao waliamua kuingia mitini. Ingawa Maftah hajafungiwa kwa madai kuwa bado hajaitwa kujieleza.

Lakini kinachoonekana ni kwamba viongozi wa Yanga wamewahukumu wachezaji hao kwa kutumia propaganda za kiuongozi zaidi na hawana sababu za msingi za kisomi ambazo ukiwakurupusha hata sasa wanaweza kukuambia ukaridhia.

Mazingira hayo ndio yanafanya wadau wa soka na wenye upeo mkubwa kwenye masuala ya kiuongozi waamini kwamba wachezaji hao wametolewa kafara ili kulinda maslahi ya viongozi mbele ya wanachama, ambao wiki chache zilizopita walikuwa wanavurugana wenyewe kwa wenyewe.

Hakuna mwanamichezo asiyeelewa kwamba mpira ni mchezo wa makosa na huwezi kuwa juu siku zote ndio maana kukawa na usiku na mchana, hakuwezi kuwa mchana tu siku zote. Mbona Lehman wa Arsenal amefungwa mabao ya kizembe mechi kama nne mfululizo hatujaskia amesimamishwa miezi au hata kutozwa faini.

Paul Robison wa Totenham Hotspurs ambaye kila mechi anafungwa bao la kizembe mbona hatujaskia kaadhibiwa? Tena kasajiliwa kwa mabilioni sembuse Ivo wa Tukuyu ambaye hata glovu za mazoezi ananunua kwa machinga Kariakoo?

Achana na hao Richard Micah beki tegemeo wa Manchester City (kama ilivyo Nsajigwa kwa Yanga) ambaye yeye pamoja na wenzake wamefanywa uchochoro wakapigwa 6-0 na Chelsea stanfodi briji, angekuwa Yanga ingekuwaje?

Sipingi kwamba uongozi unaweza kumpa mchezaji adhabu kama muajiri na muajiriwa lakini si hii ya miezi sita ya Ivo na Nsajigwa iliyotolewa na uongozi wa Madega, ni kuua vipaji vya wachezaji na ni ubabe pia, kufungwa na Simba sio mwisho wa Dunia. Msiendekeze kelele za mashabiki wachache ambao wana maslahi yao.

Achana na umuhimu wao Taifa Stars, inawezekana kuna makosa yamebainika kwa utashi wa viongozi lakini kwanini wasingepigwa faini au kukatwa mshahara kwa miezi hata miwili kama inavyofanywa kwenye nchi zilizoendelea kuliko kutoa adhabu kama tunazoshuhudia ambazo siogopi kusema ni za kizamani na za kienyeji.

Halafu isitoshe viongozi hao hao wanakwenda Tiefuefu kuomba kipa wao aliyefungiwa mechi sita, Benjamin Haule afunguliwe ili wamtumie kwani ni hatari kubakiwa na kipa mmoja (Jackson Chove) ambae baadhi wanadiriki kumuita “namba tatu”. Kwani wakati mnamfungia Ivo hamkujua hilo na huyo?

Imefika wakati viongozi wa klabu za Tanzania kubadilika kifikra na kufanya mambo kisomi badala ya kutumia propaganda. Siwafundishi wajomba hizo ni salamu zangu kwenu.

Maximo sawa bwana-Ndabila


MSHAMBULIAJI tegemeo wa Prisons, Yona Ndabila amesema hana bahati na timu ya Taifa na wala hadhani kwamba anaweza akawemo katika miaka ya hivikaribuni.

Kauli ya mchezaji huyo imekuja siku chache baada ya kocha Marcio Maximo kutangaza kikosi cha Chalenji huku akiwa hayumo licha ya wadau wengi kushinikiza awemo.

“Timu mi naona ni nzuri, lakini mi naona kama sina bahati kabisa kipindi hiki kwa jinsi mambo ninavyoyaona,”alisema mchezaji huyo mwenye mabao manne kwenye Ligi Kuu ya Bara inayoendelea.

“Wakati huu ndio naona nipo kwenye fomu sana na ndio ilikuwa kipindi changu cha kulitumikia taifa kwa kila hali.

“Lakini ndio hivyo, labda ipo siku hii ni kazi yangu ngoja tupambane na Ligi Kuu kwanza tuone,”aliongeza mchezaji huyo mfupi kiasi mwenye maneno mengi.

Wa mnyama saba hawamo kambini

WACHEZAJI saba tegemeo wa Simba ya Dar es Salaam hawamo kwenye kambi ya mazoezi ya timu hiyo mjini Morogoro.

Simba yenye pointi 15 ikishikilia nafasi ya nane inacheza na Polisi Dodoma kesho mjini Dodoma katika mechi ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara.

Habari toka ndani ya kambi hiyo zinasema kuwa wachezaji hao watano kati yao waliondoka kambini juzi mchana na jana walionekana katika mitaa mbalimbali za Dar es Salaam wakiendelea na mitikasi yao.

Wachezaji ambao waliondoka kwenye kambi hiyo juzi ni Joseph Kaniki, Haruna Moshi ‘Boban’, Mussa Hassan Mgosi, Soud Abdallah,Nurdin Bakar na Moses Odhiambo wakati Akilimali Yahya bado hajapona.

Monday, October 29, 2007

Soggy Doggy dabo dabo

SOGGY Doggy ambaye amekuwa kimya kwa kipindi kirefu amesema ameamua kuachia nyimbo mbili mpya kwa mpigo ili kujenga heshima na hahofii chochote.

Msanii huyo hajavuma mwaka huu baada ya kukaa kando ya fani hiyo na kujihusisha zaidi na shughuli za utangazaji.

Alimdokeza mzee wa kutibua kwamba nyimbo hizo ambazo ni ‘ICU’ na ‘My baby’ zipo katika ubora mzuri na amezitoa kwa makusudio maalum.

“Hakuna msanii ambae ameshafanya kitu kama hicho nataka nianze kwa mara ya kwanza, wale wa kujirusha hii ya ‘My baby’ ndio saizi yao iyo nyingine imetulia kidogo.
“Ni nyimbo ambazo zina utofauti sana kwa vile nimezifanyia kazi muda mrefu wakati nilipokuwa sisikiki, zipe muda kidogo nizisambaze baada ya wiki mbili utaskia makali ya Soggy yule yule,”alisema msanii huyo.

Saturday, October 27, 2007

washkaji vipi ndio kizenji au?


jamaa hao bwana wa zecomedy wamebanwa sehemu wakinanihiii

Fanyeni fasta ujue mi dakika zangu zinahesabika



TOTTENHAM Hotspur imemteua mshambuliaji wa zamani, Clive Allen kuwa kocha wake wa muda baada ya kumtimua Martin Jol muda mfupi baada ya timu hiyo kufungwa mabao 2-1 na Getafe katika mechi ya Kombe la Uefa juzi usiku.Allen atakuwa na kibarua cha kwanza kesho atakapoiongoza Spurs kuvaana na Blackburn Rovers, ambayo kwa sasa inafanya vizuri.

Banza ni mkwara au kweli?


MWANAMUZIKI Banza Stone ambaye ni kiongozi wa bendi ya Bambino Sound Original, aliyoifufua hivikaribuni amesema kuwa anasuka bendi imara na itakayokuwa mfano wa kuigwa Tanzania.

Banza aliifufua bendi hiyo wikichache zilizopita baada ya kujitoa Twanga Chipolopolo na tayari ameshaanza maonyesho ya utangulizi ingawa anatazamia kufanya uzinduzi Novemba 3 jijini Dar es Salaam.

Msanii huyo alisema kuwa anakiamini kikosi alichonacho hadi sasa na ameridhishwa na kiwango cha kila msanii lakini anajipanga zaidi kuhakikisha anakuwa na msingi imara.

Friday, October 26, 2007

Maximo huyo Nsajigwa katoroka kempu


Maximo itabidi umpe displini huyu chalii


WACHEZAJI wanne wa Yanga wametoroka kambini huku uongozi ukilaumu wachezaji kuwa walicheza chini ya kiwango na kusababisha timu kuendeleza uteja kwa Simba.

Wachezaji hao, waliotoroka kambini mara baada ya Yanga kufungwa bao 1-0, ni kipa Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa, Amir Maftah na Benny Mwalala.

Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega alisema jana kuwa uongozi hautakimbilia kuwachukulia hatua hadi hapo utakapokutana nao na kuwasikiliza.

Nyie endeleeni kama hamjala za uso

KULENi tano! Wanangu wote mnaonicheki maeneo haya ya kujidai mida hii, mimi niko pisi sana masela na maishu yanaenda kimtindo mtindo.

Si unajua tena laifu la kiutu uzima linavyokuwa mvi zikishatanda kwenye injini ya juu? Ni kukomaa na vijana wa siku hizi ilimradi ukitinga jioni makidi wapokee kitu kumkono waringe kwamba na mshua wao kumbe zimo, si unajua za kivile?

Mwanangu mtu mzima ukiibuka na maulaji ulaji, basi striti yoteee... ngoma iko hewani vibaya sana, mpaka mtaa wa saba kwa kina nanihii wanajua jamaa mambo safi. Si madogo washafikisha, ndio usupastaa wa mtaani kwetu huo wana.

Kidogo kidogo tayari ushaingia kwenye sistimu na mambo fulani yanakaa poa Bongo, mkwanja unaanza kumwagika, madili kwa sana tu! sio ishu kupiga mayenu mpaka shingoni ukatize site senta na mabaunsa kibaa...oo!

Mkwanja kibao unahangaiika…! Si uite masela uwapige mtungi wa maana wakupage ramani kibingwa tu..!

Simpo kichizi, wala si lazima ukauze sura Bilzi kwenye dansing floo uibue vagi ukawafaidishe machizi wanaochukua dondoo za manyuzi ya udaku, halafu moningi ukaanza kuona soo kuibuka kwa wakwe.

Sam taimsi ishu tafu bongo lakini ndio ivyo wani deyi yesi, ingawa wanangu fulani wa yelloo Jangwani wanadai Sa Godi anawatupa kichizi, anakuwa kapiga zake pono lile la fofofo kila wanapokutana na hao swahiba zao hapo Msimbazi.

Mei bi wanamaanisha mambo yameendelea kuwa mazito, lakini siyo kiivyo, mbona mkwanja kibao tu unamwagika evuridei mpaka vijana wamechafuka dolerii...?

Au kuna samusingi kilitokea mitaa ya Jamuhuri Stadiumu ? Mzee mzima ayi donti no enesingi bwana! Huwaiii… Kwanini, lakini!

Lakini machizi kama vipi iti izi beta samtaimzi kusteyi kivyako vyako kama Mzee wa Kutibua na Tukuyu Stars ya kijijini kwao, hayo matimu ya kina nanihii presha tupu. Boli lenyewe la kibongo miyeyusho tu hili, mkwanja kibao bado mtu mzima unateseka tu. Huwaiiii…!

Lakini ebu kula ganzi kwanza kidogo nikuambie kitu, nyeti za vijiweni ntakupa baadae kidogo. Kwanza tuwape shavu Yanga kwa kunasa makocha watasha ambao tayari Mzee wa Kutibua na wenzake waliokuwa wakiangalia runinga wamewashuhudia wakishuka hapo kwenye hicho kiwanja maeneo ya Vingunguti.

Halafu isitoshe tukawaonyesha laivu ndani ya Jamhuri Stadiumu juzi. Masivii yanaonyesha ni bonge ya matekinishiani wala Mzee wa Kutibua na wadau wengine wa soka ambao kwa nyadhifa zao wamepata nafasi ya kuperuzi hawana noma ndio maana hatujawasoma wakibonda.

Ingawa bado hatujaambiwa kama Waserbia hao, Kondic Dusan (Mkuu) na Spanso Solokovski hatujanyetishiwa kama wameshamwaga wino kwenye kontracti lakini viongozi wa klabu hiyo pamoja na wanachama wana kazi kubwa ya kufanya.

Ujio wa hao madingi (wako kwenye siksite samsingi kwani hujui!) ni mwanzo mpya na mzuri wa mafanikio kwa vile wana uzoefu na nchini za kiafrika, lakini haimaanishi kwamba ndio kila kitu tayari.

Miezi si mingi jamaa mmoja mzungu walikuwa wanamuita Micho naye alikuwa mitaa hiyo ya Jangwani lakini pamoja na uswahili wake, akaingia mitini kiaina na kumuacha kila mmoja akisema lwake.

Lakini huyo mzungu ambaye mashabiki wengi hawakudhania kwamba angeweza kuchomoka veere suuni…, baada ya muda aliibuka kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti hili akidai kwamba anataka kufanya kazi kwenye klabu ambayo yeye “atatekeleza majukumu yake ya kiufundi tu kama kocha kuliko kuhangaika na mambo mengine”.

Kauli hiyo pekee imebeba maana nyeti ambayo viongozi wa Yanga wanapaswa kuifanyia kazi na kujipanga upya kwa kutengeneza mazingira mazuri ya kazi ambayo yatasaidia wataalam hao wanaolipwa ghali zaidi nchini kuweza kutimiza malengo yao.

Vinginevyo mamilioni wanayolipwa yatayeyuka na yatakuwa hayana maana kwani zoezi la kuingia mitini lililowahi kufanywa pia na makocha Wabrazili wawili wa Simba hata na Msauzi Trott Moloto yataendelea.

Si wakati wa viongozi kuendeleza migogoro ya ndani kwa ndani ambayo inaweza kuvuruga wachezaji na kuanza kuhujumiana. Ni wakati wa kujenga mustakabali mpya haswa kwa kuangalia Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa mwakani, tumechoshwa na hadithi za 'haikuwa bahati yetu'.

Wachezaji nao watunze vizuri na kusiwepo na matabaka ambayo yanaweza kujenga hisia wala mianya ya mkato wa tamaa.

Wanachama na wenyewe pia wanapaswa kuacha chokochoko zisizo na msingi na kuzingatia zaidi maslahi ya wengi, kuanzisha vurugu kwa lengo la kuitwa na kibosile fulani upewe kitu kidogo haijengi na hii si karne ya kuishi kwa kutegemea klabu, badilikeni.

Hata mashabiki na wenyewe wasitegemee mambo ya mteremko na waache jazba, wabadilike wawape nafasi wataalam wafanye mambo yao, wao wabaki kushangilia jukwaani tu.

Haya bwana! tuishie zetu kwenye minuso ya wikiendi, wenye uroho wa kitimoto kama Munyuku (sijasema!) wapige kwa tani yao kama Mgiriki huko Meeda ambao kwa mujibu wa kalenda ya Mzee wa Kutibua siku kama hizi bado ni muafaka za kutumbua kilaji mpaka majogoo.
Lakini msifogeti pia Zee la Kutibua lipo kwenye blogu; zeewakutibua.blogspot.com) ingawa wanazuoni waliojitolea kufanikisha zoezi hilo wanamuambia bado mchakato unaendelea muda si mrefu everisingi will bi oluraiti bila chenga.

Mukandila Tshitenge Kabanda:Im very sorry Yanga


Kaka kuna pua ya mtu nini?


ENGLAND ilivyofungwa wiki chache zilizopita na Russia 2-1 kwenye michuano ya kuwania kufuzu Euro 2008, nahodha wao Steven Gerrard aliwaambia Waingereza “samahani” huku kocha wake, Steve Mclaren akisema "Mnilaumu mimi."

Lakini kwa mara ya kwanza kwa mastaa wa kimataifa nchini Tanzania, mshambuliaji ghali wa Yanga, Mukandila Tshitenge Kabanda amewaomba radhi maelfu ya mashabiki wa klabu yake kwa kushindwa kuifunga Simba Jumatano mjini Morogoro kwenye pambano la Ligi Kuu ya Bara.

Yanga licha ya Sh milioni 50 ilizokuwa imepewa na mfadhili wake, Yusuf Manji ili iifunge Simba ilishindwa kutekeleza azma hiyo na kujikuta ikikubali kipigo cha bao 1-0 lililofungwa na Ulimboka Mwakingwe dakika ya 30 kwa shuti kali ambalo lilimpita kwapani kipa wa Stars, Ivo Mapunda.

Kabanda, ambaye aliumia baada ya kugongana na kipa wa Simba, Juma Kaseja alisema kuwa alikuwa amepania kuipa ushindi yake na alikuwa na tamaa ya mabao lakini mambo yakamuendea vibaya.

“Naomba wanisamehe tu kwa kushindwa kuwapa ushindi na kufunga magoli, sikufanya kusudi nilikuwa na tamaa sana na hamu ya kufunga magoli,” alisema Kabanda(mwenye rasta anayeangalia mbele) ambaye kabla ya kutua Yanga alikuwa APR ya Rwanda.

“Nilikuwa nimepania kucheza kwa nguvu zangu zote kuhakikisha kwamba timu yangu inashinda kwa vile nilikuwa najua ndio zawadi pekee ya mashabiki na viongozi wangu.

“Lakini hatukufanya kusudi, naomba watuamini ligi bado ni ndefu hii ni mechi ya kwanza tumekutana na hawa Simba tutakutana nao bado kuna mechi nyingine tukiwakuta tutawafunga tu, tutakuwa tumebadilika zaidi hakuna kukata tamaa.

“Na mimi na miaka miwili ya kukaa Yanga, sasa bado sijamaliza hata mmoja wa kwanza nitabadilika tu na nitaanza kufunga magoli, nimepania sana lakini bado sijapata bahati ya kutekeleza azma yangu.
Aliumiaje? : Kaseja aliruka juu wakati anaokoa mpira akanigonga na goti kwenye shingo, niliumia sana yaani nilisikia kichwa kinauma, shingo inauma, kizunguzungu ndio maana wakanipeleka hospitali.
“Siwezi kusema kwamba ni kusudi, siwezi kujua lakini mimi namuamini Mungu ndie anajua na naamini kwamba ni hali ya mchezo tuu imetokea bahati mbaya na inaweza kumtokea mtu yoyote yule anayecheza nafasi kama yangu.

Hawa Prisons ni noma wanabonda tuuuu


You Guys mko siriaz au ndio mnatuyeyusha


LICHA ya kupoteza mechi moja na kutoa sare mbili ugenini huku ikiendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Bara, Prisons imedhihirisha kwamba bado ni bora kuliko timu yoyote.

Klabu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Magereza katika mechi zote kumi ilizocheza hadi sasa inashabihiana na Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Toto Africa na Coastal Union kwa kitu kimoja tu; mabao nane ya kufungwa.

Prisons imeshinda mechi saba, sare mbili na kupoteza mchezo mmoja rekodi ambayo haipo kwa timu yoyote inayoshiriki michuano hiyo hata Simba na Yanga zenye wachezaji ghali na maarufu.
Mbali na hilo, Prisons ambayo kocha wake ni Juma Mwambusi, imepachika mabao 18 ambayo hayajakaribiwa na timu yoyote labda Polisi Dodoma na Kagera Sugar zenye mabao 10 kila moja.
Timu hiyo ambaye imekuwa ikisifika zaidi kwenye upande wa kiungo, ina pointi 23 ambazo inaweza kuziongeza itakapocheza na Moro United keshokutwa.

Washambuliaji wake, Oswald Morris anaongoza kwa ufungaji akiwa na mabao sita, huku Yona Ndabila na Said Mtupa wakiwa na mabao manne pia, sawa na Mike Katende wa Kagera Sugar.

Wachezaji wengi wa Simba na Yanga wanadai kuwa timu hiyo ilikuwa ikishinda kwa vile imecheza mechi nyingi kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Sokoine, Mbeya, lakini sasa itaanza kupata vipigo ikianza kutoka ugenini.

Tayari Prisons imepoteza mchezo moja dhidi ya Kagera Sugar.

Dube anazikwa Kesho meeeeeeeen(oct.27)


Jamaa anazikwa kesho. Media Stop.


The funeral of reggae singer Lucky Dube will be a private affair, family spokesperson Arnold Mabunda said on Monday.

"The family requested that the funeral be a private matter due to Lucky's beliefs and the church's request.

"They have requested that it not be turned into a circus, so media will not be allowed. That's not what Lucky would have wanted," he said.

Dube, a Shembe worshipper, was shot dead during an apparent hijack attempt last week while dropping his two teenage children at his brother's house in Rosettenville.

rest in peace meeeeeeeen


One love meeen, Rest in Peace tuko nyuma yakoooo
Remember Me Lyrics


chorus:


Daddy where ever you are remember me

In what ever you do I love you

Daddy where ever you are remember me

In what ever you do I love you

You left for the city many years ago

Promised to come back

And take care of us

Many years have gone by now

Still no sign of you

DaddyMother died of a heart attack

Many years ago when she heard

That you were married again

Now, I' m the only one left

In the family


Chorus:Wandering up and down

The streets of Soweto

No place to call my home

I tried to find you

Many years ago

But the women you' re married towas no good at all


Chorus:Daddy yo!!!


Thursday, October 25, 2007

sasa sijui nifanyejeee

Yaani hata siamini hawa kina Kabanda wanachofanya.....
sasa sijui tufanyeje hesabu zooote zimekwisha, halafu hawa jamaa wako kumi tu uwanja sisi tuko kumi na mmoj

a sasa itakuwa fedheha hii Siwa yaani hiii sijapata kuona. Au tumuingize Sunguti labda. mambo yamechafuka halafu zimebaki dakika kama tano tu.

Yanga....This is too much


Yanga Looooooooooooh Too much wazeeeee


SHILINGI milioni 50 walizopewa na mfadhili wao, Yusuf Manji hazikufaa kitu mbele ya wachezaji pungufu wa Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Bao la Ulimboka Mwakingwe(MWENYE UZI MWEKUNDU NYUMA YAKE NI LULANGA MAPUNDA) alilofunga dakika ya 30 lilitosha kuipa Simba ushindi wa bao 1-0 na kuifanya ifikishe pointi 14.

Simba ikiwa na wachezaji kumi baada ya beki wa kati, Henry Joseph kupewa kadi nyekundu dakika ya 15, ilipata bao hilo baada ya Ulimboka Mwakingwe kupewa pasi na Nurdin Bakari na kabla ya kufunga winga huyo mfupi alivuta hatua mbili akapiga shuti kali ambalo lilipita kwenye kwapa za Ivo Mapunda na kugonga mwamba kabla ya kujaa nyavuni.
Mchezo huo ulifanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na kuhudhuriwa na mashabiki wengi wakiwamo wengi kutoka jijini Dar es Salaam.

Manji ambaye yupo nchini Marekani aliwapa Yanga Shilingi milioni 40 kwa ajili ya maandalizi ya mechi hiyo huku akiwapa wazee Sh milioni kumi za kufanyia 'shughuli' za maandalizi.
Mchezo huo ulichezeshwa na Othman Kazi wa Dar es Salaam aliyesaidiwa na Samuel Mpenzu wa Arusha na Ismail Mshana wa Dodoma.

Ulikuwa ni mchezo wa tatu kwa Kazi kuchezesha mechi ya Simba na Yanga tangu awe mwamuzi na Yanga haijawahi kushinda akiwa yeye mwamuzi.

Mechi nyingine ambazo Kazi alizochezesha kati ya Yanga na Simba ni Simba iliyoifunga Yanga 2-0 katika fainali ya Tusker Julai 2, 2005 jijini Mwanza na nyingine ni ya Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo iliishia kwa suluhu jijini Dar es Salaam Machi 26 mwaka jana.

Simba walimrudisha katikati Said Sued na kumpeleka Kelvin Yondani katika nafasi ya beki wa pembeni, huku Nico Nyagawa pia akirudishwa katikati kusaidia baada ya kutolewa kwa Henry Joseph ingawa kipindi cha pili Sued alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Soud Abdalla.
Simba ilianza kwa kushambuliwa na ndani ya dakika ya saba, walikuwa tayari wameruhusu kona mbili ambazo hazikuzaa matunda.

Hata hivyo katika mchezo huo, Simba wanapaswa kumpa shukrani kipa wao, Juma Kaseja ambaye alifanya kazi ya ziada kulilinda lango lake.

Shadrack Nsajigwa alipiga kona dakika ya saba, lakini Thomas Morris alipotaka kufunga alijichanganya na kuutoa nje mpira.
Hata hivyo Simba ilijikuta matatani baada ya beki wake wa kati, Henry Joseph kupewa kadi nyekundu na mwamuzi Othman Kazi kwa kumchezea vibaya Thomas Maurice.

Dakika mbili kabla ya mapumziko, Laurent Kabanda angefunga bao, lakini mwamuzi alilikataa mpira uliokuwa umeingia wavuni kwa sababu kipa wa Simba, Juma Kaseja alikuwa amepigwa mtama na wachezaji wa Yanga.
Mechi hiyo ambayo ilihudhuriwa pia na kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo ilishuhudiwa Simba ikienda mapumziko ikiongoza kwa bao moja.

Kipindi cha pili, Simba ilijaza wachezaji wengi nyuma kujihami jambo ambalo lilifanya 'kuzidiwa' mara kwa mara na Yanga ambayo nayo iliamua kupeleka wachezaji wengi kushambulia.
Hata hivyo kujipanga vizuri kwa wachezaji wa Simba kuliwafanya Yanga washindwe kuingia ndani ya eneo la vijana wa Msimbazi ambao waliongezewa nguvu na Julius Mrope aliyekuwa akisumbua sana.
Kabanda wa Yanga aligongana na Kaseja katika moja ya hekaheka na kufanya apelekwe hospitalini.

Yanga ikicheza bila Ben Mwalala na Athuman Idd waliofungiwa na TFF, wameshindwa kulipa kisasi cha kufungwa na Simba kwa takribani miaka mitano.
Mpambano huo ulikuwa ni wa 24 tangu mwaka 2000 huku Simba ikiwa na rekodi nzuri ya kushinda mechi 13 pamoja na ya jana na Yanga imeshinda mara nne tu.
Dakika ya 53, Yanga walitaka kulazimisha bao la kusawazisha baada ya washambuliaji wake kumpora mpira Kaseja na kufunga, lakini mwamuzi alikataa.

Yanga: Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa, Lulanga Mapunda, Yusufu Hamisi, Wisdom Ndhovu, Credo Mwaipopo, Amri Kiemba/Mrisho Ngassa, Waziri Mahadhi, Laurent Kabanda, Thomas Maurice/Abuu Ramadhani, Amir Maftah/Aime Lukunku.
Simba; Juma Kaseja, Said Sued/Soud Abdalla, Nurdin Bakari, Kelvin Yondan, Henry Joseph, George Owino, Nico Nyagawa, Shaaban Kisiga/Mohammed Banka, Mohammed Kijuso/Julius Mrope, Joseph Kaniki na Ulimboka Mwakingwe.

Friday, October 19, 2007

Rooney na Yona Ndabila wa Tukuyu

WASHKAJI zangu inakuwaje kuwaje hapo...! Ishu za 'saa ya inzi na teke la gia' zikoje? Jamaa waliomwendea hewani Mzee mzima wikiendi iliyopita walimpa maripoti ya kumwaga.

Kuna miguno lukuki ya kichinichini, wanangu fulani wanasema wanaskilizia maumivu kutoka na matanuzi ya Idi, masimbi yametoweka ghafla mifukoni na mizinga ndio kibao ili mradi huko Samora na Kariakoo kuendeke watu wakasake lami.

Ndio ukubwa huo…, jamaa wa ukanda wa Oldonyo Lengali wanakuambia "imekula kwako full arifu" .
Wikiendi kama hii, iliyopita ni ya neema kwa Mzee mzima wa kutibua kwenye mambo ya minuso kwa vile alikuwa amejikita kwenye viwanja fulani vya wateule kwa mialiko maalum , ni mitaa ya pembezoni mwa jiji la Kandoro. Mambo ya kuzama midomoni yalikuwa si ya kitoto hapo. Siunajua tetemeko la watu wazima wakivamia fani zao?

Mzee wa Kutibua alikuwa akijipongeza na washikaji zake ambao walifanikiwa kukazia mpaka mwisho, ingawa baadhi kwa taaaaabu na ushahidi anaona kwa vile si mara moja aliwakumbana kwenye viepe wakijiita Philipo badala ya Salehe au Ojuku. Wala huyu jamaa aliyekuja kubanana na mimi hapa kushoto kwangu sijamtaja.

Kiwanja alichoibua wa Kutibua kama kawa kilikuwa na mtu kibao zilizopiga mijusi ya kufa mtu, kila mteule alikuwa akifyonza kwa upana wa domo lake mwanangu na sura fulani fulani zikiwa za hao wanabongofleva pia.

Wakati watu wazima wakiendeleza makamuzi kimtindo, Mzee wa Kutibua akaanza kukumbuka misemo ya waliopiga buku longi taimu huko lasti yiazi kwamba ukitaka kupata nyeti za mtu mzima mtwange kilauri kifike mahala pake.

Jinsi taimu zilivyokuwa zikiyeyuka kauli za wale mlioita Wahenga zikaanza kuthibitika 'laivu' baada ya waliokuwa wakijifanya wapole kuanza kucharuka kwa kutoa stori za kila sampuli.
Si baadhi yao wamezoea maji ya machungwa Stiazi? Mmoja aliyekuwa amenyonga mjusi wake ambao anadai kauibua dukani huko Samora kwa jiwe kadhaa kashauvua kaupiga mezani na shati alilokuwa akilinadi kanunua kilo limechomolewa saidi moja linaning'inia.

Kando kando waliobana na kina mamananihii wao tayari wameanza kupata burudani kwani mwanabongofleva (tumsitiri kwa jina) mmoja ambaye ni swahiba kinoma wa Mzee wa Kutibua ameshaanzisha tafrani ambayo hata fidifosi wa bwana Mwema hawaiwezi, si maji yamevamia oblongongata!

Kalipua bomu kwamba amempiga kitambi waifu wa mshikaji mmoja ambaye ni miongoni mwa wawezeshaji wa mchakato wa Bruwarizi kwenye hiyo mitingi inayoendelea, jamaa kusikia kukachafuka huku wazee wa udaku wakinyemelea kando kando kutaka kunasa hili na lile.
Mzee wa Kutibua ambaye ni muoga wa manundu ya kujitakia, mida hiyo yuko na nanihii zake kadhaa kichwani, kashapotea kwenye uwanja wa mapambano ili kuwaacha walioshiba watengenezane na hata ikiwezekana baada ya siku tuskie singo mpya imetoka kwa ‘Bonyeza’ hapo Morocco au kwa ‘Matawi’ Mikocheni. Ndio inavyokuwa kwa wanabongofleva wenu! Unashangaa….. kwani hujaskia huyo aliyetunga eti “yuko Bar wife asimtafute”! Huwaiiii…?

Labda tuchenji chaneli. Lakini hivi kama mnataka ndondi simuingie gyimu mmalize kazi tuwaunganishe kwenye listi ya Matumla na swahiba yake Cheka? Ndio maana yake kwani sisi tumewaambia uwanjani tunakuja kuangalia ngumi sisi!

Mmepewa vichwa mkapitiliza sasa mmeamua kugeuza na uwanja wa soka sehemu ya mapambano baada ya kuona mambo yamekuwa mazito.

Upuuzi huo wa baadhi ya wachezaji wakiongozwa na hao wa hizo zinazoitwa Simba na Yanga umekuwa ukijitokeza kwa kiasi kikubwa katika wiki chache zilizopita ambapo bila ajizi na waamuzi nao wamekuwa wakigawa redi kadi na yello kama njugu, kitu ambacho pia kimekuwa kikichanjia kuharibu ladha ya Ligi Kuu hii ya Bara.

Utovu wa nidhamu kwa wachezaji sasa umeonekana kupitiliza kutokana na kutofuata taratibu, kanuni hata sheria zilizowekwa. Au ukisajiliwa ukipewa Baluni na geto la chumba kimoja tena uswazi ndio umefika mwisho kila kitu kipo chini yako? Ni dalili za kuchuja kama hamjui masela.

Sifa za kijinga za uwanja wa Jamhuri au Taifa hazikusaidieni, badilikeni mcheze soka kwa kutuliza mpira chini na kufuata maelekezo Nainte minitsi, utovu wa nidhamu na ukorofi hausaidii.

Haya mangumi uwanjani, kupigana hovyo, matusi na kuumizana bila sababu za msingi hakuwajengi, hakuna anayekwenda uwanjani kuangalia nani atamkunja nani au nani mbabe wa nani, tunataka kuona futiboli badilikeni mtushawishi angalau tuanze kufikiria kuachana na hao wa kina Rooney na Terry wa England tumuangalie Yona Ndabila wa Tukuyu. Kwani wana tofauti gani?

Mwenye akili timamu ataelewa anachonena Mzee wa Kutibua, hayo mambo ya ubabe waachie hao wanaoitwa makomandoo wapambane na wanaowajua wao kusaka hizo buku za geti koleksheni!

Hata propaganda za kiuongozi haziwahusu kabisaa…, kazi ya mchezaji ni kucheza soka ili mradi uwe unalipwa kilicho halali yako vijana na mama nanihii apige viwalo vya maana.

Wala suluhisho la kuboreshewa maslahi au kutekelezewa mambo yenu si kwa timu kufungwa au kutoa sare, mwisho wa siku nyie wachezaji wenyewe ndio mnajiharibia, viongozi ni watu wa kupita tu leo na kesho hawapo nyie timu ikiboronga nap engine kushuka daraja wakala gani atakuangalieni? Au atakayeelewa sababu zenu za Kiswahili eti kwamba mlitibua ili Mwaisakandu atimuliwe na wanachama.

Soka ni laifu yenu wanangu na mnapaswa kulisukuma kiukweli, hamkereki na hivyo vikwapa vya makonda, ifike mahali na nyie mjitume zaidi muishi maisha mazuri na mkwee huko ughaibuni wanakovuna dola wenzenu.

Kubalini kubadilika kifikra na muangalie wanachofanya wenzenu walioendelea, wanangu mjenge utamaduni wa kujifunza na kwenda sambamba na mabadiliko ya huko ‘Duniani’.

Hata Marefa na wenyewe wanapaswa kuwa makini zaidi kuepusha ndondi na rapsha baina ya wachezaji bila sababu za msingi na ambazo zinaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuvuruga saikolojia na kuharibu mchezo.

Zingatieni sheria na muwe makini zaidi si kugawa kadi ili mradi tu. Siyo kwamba hatujui, tunajua mpo mnaovuta mapene na kupindisha mambo tumeshawapa tipu Takukuru wako mitaani.
Ayaaah….! kabla sijaingia mitini! Wanangu wa mji kasoro Bahari, Jeitano nipo ndani ya stadiumu kushuhudia watu wazima mzigoni, mwisho na mwanzo wa ubishi mpya. Mwekundu au Wanjano atacheka? Kazi kwao!
Haluu...! linakuja Libulogi la Mzee wa Kutibua ni funika bovu, Bongo nzima hakuna! unaweza ukalichungulia hata mida hii kama vipi (mzeewakutibua.blogspot.com) lakini kuwa mpole linasukwa na wanazuoni wa hapo Mlimani.

Simba Yanga acha wauwane j5

Simba na Yanga ni jumatano Moro, jamaa fulani naskia wamepewa milioni kama 50 hivi kwa ajili ya kufanya mambo fulani. TAKUKURU Mpoooooo! Kazi kwenu.

Dah! mwanangu Lucky Dube kadedi kabisaaa!

Wamempiga Risasi jamaa
JOHANNESBURG, Afrika Kusini
WAPENZI wa muziki wa Afrika Kusini jana walikuwa katika siku ya majonzi kutokana na kifo cha kushtua cha mwanamuziki wa reggae, Lucky Dube, 43, aliyepigwa risasi na majambazi waliotaka kumpora gari usiku wa kuamkia jana maeneo ya Rosettenville, Johannesburg.
Msemaji wa Polisi wa Afrika Kusini, Cheryl Engelbrecht alisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 8:20 usiku wa kumkia jana wakati mwanamuziki huyo nyota alipokuwa akiwashusha watoto wake wawili katika nyumba ya ndugu yao.
Mwanamuziki huyo alikuwa akiendesha gari lake la kijivu la Chrysler akiwa amewapikia watoto wawili.
Msemaji huyo wa polisi alisema Lucky Dube alikuwa tayari amewashusha mtoto wake wa kiume mwenye miaka 15 na binti yake mwenye umri wa miaka 16 wakati alipovamiwa na majambazi waliokimbia baada ya tukio hiklo wakiwaacha watoto hao bila kuwajeruhi.
"Mtoto wa kiume alikuwa tayari ameshuka kwenye gari. Alipoona tukio hilo alikimbia kuomba msaada" alisema Engelbrecht.
Lucky Dube akiwa amejeruhiwa alijaribu kuondoka gari kwa kasi ili asipigwe risasi nyingine, lakini alipoondoa gari hilo aligonga mti na kufa hapo hapo.
Polisi wa Johannesburg wanawatafuta
watu watatu wanaoendesha gari la bluu Vokiwageni Polo (VW Polo) ambao wanadaiwa kuwa ndio waliomuua msanii wa huyo.
Miongoni mwa watu wa kwanza kufika katika tukio ni wanamuziki wenzake, Mzwakhe Mbuli, Ringo Madlingozi na Deborah Fraser.
Mbuli alisema: "Ni jambo la kushangaza, wakati nchi inajiandaa kwa fainali za Kombe la Dunia za rubgy, tunapatwa na tukio hili la kusikitisha. Tutashangilia vipi katika hali ya majonzi namna hii, nadhani polisi wanachimba na kuwakatama majambazi hawa."
Mashuhuda walisema kuwa watekaji hao walifungua mlango wa gari na kumpiga Lucky Dube risasi mbili.
"Lucky Dube alijaribu kuondoa gari na akagonga mti na kufariki," alisema shuhuda mmoja na tayari studio ya kurekodia iliyokuwa inamilikiwa na Lucky Dube, Gallo Records imetuma salamu za rambirambi.
"Alikuwa mpole, alikuwa anazungumza taratibu na rafiki mkubwa," alisema Ivor Haarburger, ambaye ni Mkurugenzi wa Gallo Records.
Haarburger alisema Lucky Dube alikuwa mwanamuziki bora reggae bora duniani na aliyekuwa na mashabiki wengi kimataifa nje ya Afrika Kusini.
"Alikuwa mkubwa hata nje ya Afrika, alikuwa anavuta watu 40,000 mpaka 50,000 katika shoo mmoja," alisema Haarburger.
Alisema Lucky Dube amekuwa akizunguka nchi mbalimbali duniani kutangaza albamu yake mpya ijayo ambayo ndio ilikuwa ipo njiani kurekodiwa katika studio hiyo.
Lucky Dube, alizaliwa mwaka 1964, na kupewa jina la "Lucky" kutokana na kuzaliwa akiwa na afya mbovu na madaktari walidhani angekufa siku chache baada ya kuzaliwa.
Lakini Lucky Dube aliishi na kuwa kijana aliyekuwa mstari wa mbele katika muziki wa reggae uliotetea haki za weusi dhidi ya ubaguzi wa makaburu wa Afrika Kusini.
Mwanamuziki huyo ambaye alikuja Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 2000 ametoa jumla ya albamu 20 na alikuwa anajiandaa kurekodi albamu ya 21.
Baadhi ya albamu zake ni Rastas Never Die, Think About The Children, Soul Taker, Trinity na albamu yake ya mwisho ni aliyotoa mwaka jana iliyoitwa 'Respect'.
Mwanamuziki huyo aliyetamba na vibao kama Remember Me, Slave na Prisoners alikuwa havuti sigara,bangi wala kunywa pombe ya aina yoyote.
Licha ya mambo yote ameshinda tuzo mbalimbali 20 ndani na nje ya Afrika Kusini.
Historia yake kwa ufupi ni kwamba Lucky Philip Dube alizaliwa Ermelo, mashariki ya Johannesburg, Agosti 3, 1964.Baada ya mama yake Sara kutaka kuitoa mimba hiyo bila mafanikio, ndipo alipozaliwa Lucky Dube akiwa na afya mbaya. Alizaliwa katika malezi ya mzazi mmoja tu mama aliyekuwa maskini asiyejiweza hali iliyomfanya aishi maisha ya tabu.Wazai wa Lucky Dube walitengana kabla hajazaliwa hivyo kumfanya mama yake kwenda kutafuta kazi sehemu nyingine na kuwaacha Lucky Dube na wadogo zake; Thandi na Patrick wakilelewa na bibi yao.

Thursday, October 18, 2007

Msikieni Banana Zorro anavyosema

Msikieni Banana Zorro anavyosema
......... Hii ni laivu amelonga na Mzee mzima hapa.

"Kinachotokea ni kwamba wasanii wengi hapa kwetu hawajaelewa umuhimu wa kutuma kazi zao kwenye kituo kama Channel O, kuna vitu vingi vinachangia lakini mi nafikiri ni uelewa binafsi.

"Halafu kwenye suala la ubora bado, wasanii wanaiga mno kila kitu kutoka nje hususani Marekani, sasa mwisho wa siku wanashindwa kuzipeleka nje kwa vile hazina jipya wala hazitofautiani na hizo zinazotoka Ulaya,"


"Unakuta msanii ana wimbo mzuri lakini ikifika kwenye suala la video anaiga kila kitu, hakuna jipya yaani, halafu na makampuni yenyewe ya kutengeneza ndio yale yale, sasa zinavyopigwa zinakuwa zinafanana kwa kila kitu na ile halisi ambayo pengine unakuta ni ya msanii mkubwa ambaye amejijenga sana.

"Silaumu watengenezaji, wasanii ni tatizo kwa vile mtu unapaswa kujua kwamba unataka nini na ufanye nini, unakuta msanii anaiga mawazo na mfumo wa video ya Kimarekani ambayo imeandaliwa shilingi labda milioni sita lakini yeye anataka kuitengeneza kibongo bongo shilingi laki tano au sita.

"Unategemea nini hapo? huwezi kupata kitu makini na huu Umarekani ndio unatumaliza kabisa tunashindwa kushindana nje na wenzetu kwa vile hakuna jipya, ndio hiyo inatokea Channel O unakuta yupo mmoja wakati bongo hapa hawana idadi.
"Matokeo yake ndio unakuta wenzetu wanazidi kupeta tu sisi tunabaki na Bongo yetu,"anasema msanii ambaye haya dingi yake ni Mwanamziki kama ulimskiaga kwenye ile Mass Media Bendi ile iliyochanaga na kupotea ghafla kila mtu akala chake.

Babu Grant si ajiuzulu tuuuuuu!

Sasa mshikaji wangu Grant......................!

UEFA wamemwondoa benchi kwa vile hana ganda(kibali), timu inaboronga.., wachezaji hawamtaki wanadai anafundisha kama ndondo za Manzese, umri umekwenda wewee.... sasa kwanini usimuachie Ten Cate tu.

Dingi yake huyo Grant unajua anasemaje? msikie..."Kumekuwa na mambo ya ajabu, watu wanapoingia uwanjani huwa wanaimba nyimbo za kumsifia Mourinho kitu kinachoonyesha kwamba Grant hakubaliki."

Mchezaji mmoja ambaye alikuwa ameshikilia viepe vyake na Bavaria yake alipomuona Mwandishi akamwambia hivi: Grant hana sifa ya kufundisha timu kubwa kama hii, tutakapocheza na timu kubwa tutakuwa tukifungwa kwa sababu yake, hana ujuzi wa kutosha,"
........... Simo.. umewaskia mwenyewe.

Monday, October 15, 2007

cooper kaja akyamunguuuuuu

Huyu hapa cooper
Mchekeshaji maarufu duniani, Mark Curry ambayeamejipatia umaarufu mkubwa katika kipindi cha Hanging with Mr Cooper atawasili jijini Oktoba 17 tayari kwa onyesho lake la kwanza Tanzania lililopangwa kufanyika kwenye ukumbi mdogo wa Diamond Jubilee (VIP) Oktoba 19.

Ze comediiiiiiii noma! Ferouzi chali nakwambia!

KUNDI la Ze Comedy limempiga bao msanii Ferooz kwa kutoa video ya wimbo wake wa ‘Bosi’.
Ze Comedy wakiongozwa na Masanja Mkadamizaji, wiki iliyopita waliibuka katika kipindi chao cha kila Alhamisi na video ya wimbo wa ‘Bosi’ ulioimbwa na Ferooz na kuwashirikisha Juma Nature na Solo Thang ambaye sasa anaishi Ireland Kaskazini.

Ferooz anasema kuwa hakutoa video hiyo kwa sababu kampuni iliyomtengenezea ilidai kuwa kulitokea matatizo katika kompyuta aliyohifadhiwa na kusababisha iungue wimbo huo ukiwa ndani.

“Sikuwa na ujanja na nikaona ni kazi tena kuanza kuwakusanya Nature na Solo ambao walitumia muda wao. Lakini pia baadaye Solo akaondoka kwenda Ulaya, lakini bado nilikuwa na wazo la kutengeneza tena video yake.

“Lakini jamaa nimeona wametoa video ambayo ukiangalia utaona ni wabunifu, si tu kwamba wameniwahi na kufanya video nzuri hata kabla yangu. Lakini wamejitahidi kuonyesha ni kitu waliochokikubali na kukifuatilia. Nimewakubali sana,” anasema.

Alipoulizwa Nature :Hata video yao imetengenezwa vizuri sana, hisia zao walikuwa utafikiri wao ndiyo Nature, Ferooz au Solo. Wamefanya vizuri mimi wamenifurahisha,” anasema Nature.

Friday, October 12, 2007

Haluuuuuuu Yanga imeibwa akyamungu.

Madega aporwa timuuuuuuuuuuuu

MGOGORO kwenye klabu ya Yanga jana ulizidi kuwa mgumu baada ya timu kuondolewa kutoka kambini Morogoro na kuhamishiwa Dar es salaam, muda mfupi tu baada ya mwenyekiti Imani Madega kuongea na wachezaji na kuhakikishiwa kuungwa mkono, huku katibu mkuu, Lucas Kisasa akisimamishwa na mahakama.

Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega na mfadhili mkuu, Yusuf Manji waliibua tofauti zao mapema wiki hii baada ya Manji kutangaza kujiondoa Yanga kwa madai kuwa uongozi umeshindwa kutekeleza zoezi la kuihamishia timu kwenye kampuni, huku Madega akisema zoezi hilo lina upungufu mkubwa wa kisheria na kikatiba na linahitaji muda.

Jana asubuhi, wachezaji waliandika barua ya kutaka kuonana na mfadhili mkuu wa Yanga, Yusuf Manji na kumuandikia mwenyekiti Madega kuwa iwapo hatamrejesha Manji mapema watagomea mechi ya Jumapili dhidi ya Mtibwa Sugar.
Taarifa iliyotumwa kwa waandishi wa habari kutoka Mkoani Morogoro ilisema wachezaji hao wameutaka uongozi huo kumrejesha haraka mpendwa wao Manji, ambaye aliwalipa fedha za usajili.
''Wamrejeshe haraka ikiwezekana leo usiku (jana) kwani ni mtu muhimu sana kwetu kwa kila kitu, tunataka arudishwe haraka kabla mechi ya jumapili,'' inasema sehemu ya barua yao.
Barua hiyo inasema maamuzi hayo ni ya wachezaji wote, ambao wamesaini isipokuwa Laurent Kabanda, Said Maulid na Thomas Maurice.
Baada ya kutaarifiwa suala hilo, Madega alienda Morogoro asubuhi na kuongea na wachezaji, ambao walimhakikishia kuwa wako pamoja naye, lakini muda mfupi baada ya kuondoka Morogoro, kocha Jack Chamangwana aliagizwa aisafirishe timu kuja Dar es salaam, ambako baadaye ilisemekana kuwa wachezaji wamewekwa kwenye hoteli ya Courtyard na Kempiski.
“Nimesikia timu imechukuliwa,” alisema Madega. “Mimi niliongea na wachezaji na wakanihakikishia kuwa hawana matatizo. Inaelekea kiongozi wa timu Emmanuel Mpangala amezidiwa nguvu.
“Lakini nitaitisha kikao cha kamati kuu ili tujadili na kufikia uamuzi. Huu sasa ni uhuni maana ni kama klabu haina timu.”
Habari zaidi zinasema kuwa mipango ilikuwa ikifanyika ili wachezaji waongee na Manji na mmoja wa wachezaji alipopigiwa simu jioni, alisema kuwa walikuwa wakielekea kukutana na mfadhili huyo.
Kuna uwezekano mkubwa, Madega na viongozi wenzake wakaomba mechi ya kesho dhidi ya Mtibwa na nyingine zinazofuatwa zisimamishwe hadi hapo hali itakapotengemaa.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Lucas Kisasa amesimamishwa na mahakama kujishughulisha na masuala ya klabu baada ya wanachama watatu – Juma Magoma, Rashid Bhinda, Godfrey Mwaipopo kufungua kesi Mahakama ya Wilaya ya Ilala.
Katika kesi hiyo, wanachama hao waliiomba mahakama imsimamishe katibu mkuu na mwanachama anayeitwa David Mwakalindile, ambaye aliajiriwa kama mhasibu wa klabu, kwa kesi ambayo inatarajiwa kufunguliwa dhidi ya wawili hao.
Katika hatua nyingine, kundi la wanachama wakiongozwa na Yusuph Mzimba wamemtaka mwenyekiti Madega kutangaza kuwa mkutano uliopangwa kufanyika Oktoba 16 kuwa ni halali kwa kuwa aliwaahidi wanachama kuwa angeitisha mkutano katika muda wa siku 45, ambazo zinaisha Jumanne.
'' Sasa siku 45 zinatimia Oktoba 16 na tena amegeuka na mwenyekiti alisema amefuta mkutano, kama kweli ni uvunjaji wa katiba na kutokana na hilo tunamuomba katibu mkuu aitishe mkutano huo kwa sababu ana mamlaka ya kuitisha mikutano yote ya klabu,'' alisema Mzimba.
Hata hivyo, Madega alisema mkutano hautakuwepo kwa sababu hali si shwari klabuni na hivyo kuitisha mkutano sasa itakuwa ni kuhatarisha amani.
“Kwanza mkutano ule ulikuwa uzungumzie katiba, lakini hakuna linalojadiliwa kuhusu katiba sasa, hivyo siwezi kuitisha
mkutano hadi hapo hali itakapokuwa shwari.

soma hapa mwanangu

Hichi kitu bado hakijakaa freshi bado kinakarabatiwa na jamaa fulani hivi zinazopiga kitabu cha kufa mtu hapo Yudiiiiiiiiiiii maeneo ya Mlimani hapo usijifanye hujui. Jamaa wanataka kutoa kitu cha kufa mtu Tanzania nzima hakuna mfano wanavyosema wao..
Endeleeni kuskilizia basi. Pamoja wanangu.

Necha kaula kinoma shavuuu nhihaaaaaaaaaaa!

MSANII maarufu wa muziki wa Rap nchini, Juma Kassim ‘Nature’ amefanikiwa kuibuka mshindi wa tuzo za Video Bora ya Channel O kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.Katika tuzo hizo zilizofanyika jana, Nature alifanikiwa kuwashinda wasanii wengine watano kutoka Kenya na Uganda na kuibuka na ushindi huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na Watanzania wengi.Aliochuana nao katika kitengo cha video bora ya Afrika Mashariki huku yeye akitumia wimbo wake wa ‘Mugambo’, walikuwa ni E.A.B.C – Kube, IDA - Make it Hot, Nameless – Sinzia, Wyre - Make A Choice (wote kutoka Kenya) huku Peter Miles - Love akiwa anatokea Uganda.Mashabiki kadhaa walijitokeza jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam kumlaki Nature ambaye aliongozana na msanii mwenzake Rich One kwenda katika tuzo hizo. Baadhi ya mashabiki hao walikuwa wakisukuma gari alilokuwa amepanda Nature baada ya kuwasili kuonyesha furaha nyao kwa msanii huyo kipenzi cha wengi.Hii ni mara ya pili kwa Nature kuwania tuzo hizo na pia aliwahi kuwania tuzo za MTV kupitia wimbo huop lakini akaambulia patupu.Msanii mwingine wa Tanzania ambaye amewahi kushinda tuzo ya Channel O ni Lady Jaydee kupitia nyimbo zilizokuwa katika albamu ya Machozi na Binti.Kwa sasa Nature ndiye kiongozi wa kundi la Wanaume Halisi baada ya kutengana na wenzao katika kundi la Wanaume TMK ambao nao kwa sasa wanajulikana kama Wanaume Original.Nature ni kati ya wasanii wanaokubalika kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kuimba aina tofauti ya muziki na wimbo wa ‘Mugambo’ ameuimba katika miondoko ya Kwaito ambayo ni maarufu sana Afrika Kusini.Ushindi wake unakuwa ni mwanzo wa ndoto zake na amewahi kutangaza kuwa kushinda tuzo hasa za nje ya Tanzania imekuwa ni moja ya ndoto kubwa ndiyo maana alijisikia vibaya aliposhindwa kutwaa tuzo ya MTV lakini hakutakata tamaa.Awali, Nature alikuwa na hofu huenda ingekuwa vigumu kushinda tuzo hiyo kutokana kuwa na Wakenya wengi ambao wengi pia waliamini huenda ndiyo walikuwa na nafasi kubwa zaidi lakini ‘akawapasua’ na kuibuka kidedea.

huyo ndiyo shetani wa Temba bwana.nomaaaaaaaaaaa

Wimbo: Mwaka wa Shetani
Msanii: Mh.Temba ft Juma Jazz
Studio: Bongo Records


Intro: Shetani shindwa kabisaaa

Verse: 1
(Temba)Tarehe moja mwezi kwanza mwaka nimesahauhuu mwaka nauita Baba, ni mwaka wa Shetani ndani ya fani ya burudanishetani x2
Akupenda maendeleo aliwagombanisha wenye vyeo na wasio na vyeo Ni historia isiyofutika kwa makundi mengi kuvunjika GangweX2Gangwe Mob ilikufa sasa imerudi, amjapatanishwa mnapatanawakati kimoyomoyo mnachukiana mii naona aina maana kwa matarudiayale yale ya mwaka wa jana,Parklane, Tng Tanga ndio kwao walipiga bao saa shetanikawageukia wao, kuna nani Tanga au kuna mwangahii siri natoboa ujue ushajiwekea doa, Gheto Boys uliongoza wewe,Watu Pori uliongoza ukaongoza wewe,tatizo nani wao au wewe

DAZ (Manunda) maji ya shingo waliimba waokamanda waliimba wao ni nyimbo za majonziziliwatoa watu machozi leo vipi mmoja wenu mnamtoa chozi Ambako amjatengana anzeni kusali leo shetani anawamega waoVichwa wanaumiza wazenji wanajiulizamlitaka kuwa naesasa tena hampo nae mmemtenga mmejitenga?
Tubery vipi, Wakali kwanza ndiyo kwanza mlikuwa mnaanzatatizo nini au kuna jini,hapo mjiniHBC kila mwaka itarudi itarudi hata Yesu alisema atarudiatarudi mpaka leo ajarudi, au mnafanya makusudimacho yangu yanaona mbali mpaka chini ya bahariMaster J na Majani hivi ni kweli hampatani au ni storiza mtaani tumtafute mchawi nanii haa

Chorus:(Juma Jazz)
Mkorofi naniiNani alaumiwee hee heemwaka wa shetaniiii
Nanii alaumiwee hee hee
Akilini mwangu mii nawazanakumbuka wapi tulipotokampaka leo tunavunjikaa


Verse 2(Temba)GWM, Gangwe, Manduli, Manyema, Wachuja Nafaka, Wanaumee (heee)Wenyewe kwa wenyewe wapinzani marasi hawagombani siku zote wanaomba amaniTMK ilianza kwa mara ya kwanza ilizaliwa mwanza mii nasimuliwa lakinisikuwepo waliniadisia wenyewe wahasisi ambao wengine wamegeuka kamamafisi,Mii wakati huo natoka jeshini nkawafuata washikaji nkawahambia naselahee(heee)Wanaume hee (heee)washikaji hee (heee)nkawahambia naombeni namba wakaniaambia huu msafara wa mamba mii mwenyemamba, wakaniambia utaweza ntawahambia jeshi nimeweza ntashindwa hapakuchezaa,Basi tukaungana tukaendeleza mapambano yasiyokuwa na mfano tnk raisalitupenda nchi nzima walitupenda kwa kuwa kulikuwa akuna timu ya kurembanii kutoka chata ni shoka wengine walishindwa wakatoka,
Sijui nini kilitokea au shetani "sijuii"au mibange "sijuiii"
labda mademu "sijuii"Ghafla nkashangaa magazeti yanahandikaa oooh TMK imevunjika ooh TMKimesambatikaa, oooh TMK kunapatashika,Mliambiwa na nani kweli huu mwaka wa shetani mpaka leo ajulikani mkorofinanii,TMK haijafa TMK kama daladala akishuka mtu anapand mtu kikitoka kitu8kinahingia kitu checheki hiki kituu,Umoja ni nguvu na hapa tumekula yamini tulajiamini TMK siku tunafukiwachini aminiii

.Chorus:(Juma Jazz)
Mkorofi naniiNani alaumiwee hee heemwaka wa shetaniiii
Nanii alaumiwee hee hee
Akilini mwangu mii nawazanakumbuka wapi tulipotokampaka leo tunavunjikaa

Intro:Haa haa kwishaa kabisa amniwezi

Ntawavuruga vuruga wotena huo mziki wenu wa bongoflevamtarudi mtaani sijui mtaenda kuwa vibakahaa haa...

Chorus:(Juma Jazz)

Mkorofi nanii

Nani alaumiwee hee heemwaka wa shetaniiii

Nanii alaumiwee hee hee

Akilini mwangu mii nawazanakumbuka wapi tulipotokampaka leo tunavunjikaa

Autro: Mkorofi nanii(shetanii)

Mwaka wa Shetanii(Shetanii)

Tiefuefu inavyoshikwa masikio

“MKOROFI nanii.. nani alaumiwee hee heemwaka wa shetaniiii…,nanii alaumiwee eee ee..Akilini mwangu mii nawaza, nakumbuka wapi tulipotokampaka leo tunavunjikaa…”Mzee wa Kutibua vipi leo? Au mkwara? "sijuii", pengine biti zimemdatishakwa Dunga, “Sijui”, au mambo ya mwisho wa mwezi? “Sijui”, labda kadata,“Sijui”.Ni maswali yanayowakaa kooni washirika wa Mzee wa Kutibua mida kama hiiwanapoperuzi ukurasa huu kutokana na vesi matata aliyoanza nayo ambayo sikawaida alivyozowea kusomeka.Lakini si uungwana kwa Mzee wa Kutibua kuanza kumwaga sera kwa washirikawikiendi hii bila kuwapa hai kimtindo kuweka mambo sawa ingawa bichwa lakehalijakaa freshi.Limejaa nyeti za kumwaga, ndio maana minywele haikai inabaki kushindilianahuko kunako kidevu jirani na domo ambalo siku hizi limekuwa likimwagabusara za kumwaga kwa mabwana wadogo huko Dasilamu mjini.Ndio mambo yenyewe ya tawni wenyewe wanasema Kibongo Bongo, kila jambolazima liwe na mikogo yake. Ndio maana hata kina Sera wameamua kung’oamabati yote kwenye hayo mabaluni na kutembelea Chesesi.Wameamua na wenyewe wabuni yao, kwani hujaona mpaka wengine siku hizi hukoShamba wanakoita Tegeta wanatinga Naiti klabu na Fusso? Wenyewe siku hiziwanaita “Flying Beds”. Aliyekuambia wanataka vigari vyenu vya kubanananani?Zao makulaji, mitungi kwa sana, kujirusha na hizo Banjuka za kina DNA hataMugongo Mugongo ngoma ikizima wanatoka nje wanaegesha kwenye Fussopanakucha.Wanyetishaji wamembonyeza na Mzee Kutibua na kumpa mchapo mpya kwamba sasaukitaka kujizolea maujiko bwana kuliko hata bwana mkubwa JK huko StetiHausi uitwe Mdebwedo.Unaweza kujikuta ukikusanya mtaa mzima ndani ya sekunde moja na utaonahata magego ya wanywa gongo ambayo siku hizi yamekuwa kivutio chawazururaji. sore Watalii. Kwani we hujaskia wengine wameanza kuhifadhiwahuko Bwagamoyo.Hao jamaa acha bwana wamejigundua kwamba ni dili ndio maana siku hizi hatawakicheka wanaziba midomo na mashati. Siku hizi Mzee wa Kutibua kaambiwahuko Tazara kwa kina Masanja wamekacha kupanda hata daladala wanazuga etini mgomo baridi kupinga hizo nauli mpya.Lakini washikaji ishu zingine lazima ifike sehemu tukubali kuwa na watuambao wana misimamo kwenye maamuzi na kuachana na ushabiki wa kizamani nakuangalia majina. Ebu niambieni, kwani hao wanaoitwa Simba na Yanga ndio kina nani kwenyenchi hii ya wadanganyika ambao hiyo Gavamenti inatuambia wanafika ‘emu34’, ukiondoa vidume wawili wa Mzee wa Kutibua walioibukia kwenye uso wadunia miezi kadhaa iliyopita ambao eti ndoto zao ni kuwa na sharubu kama Dingi yao.Kwani lazima mashindano yoyote ya nchi hii zishiriki hizo timu za hukoMsimbazi na Jangwani? Ni maswali anayojiuliza wa Kutibua ambaye kamawalivyo wadau wengine alikuwa akisikiliza mikwara ya hiyo Tiefuefu naSimba huko kwenye hivyo mnavyoita vyombo vya habari kuhusu Kombe laTusker.Simba ilikuwa miongoni mwa klabu sita zilizokuwa zishiriki michuano hiyoinayoanza leo, sijui pengine ni kwanini. lakini baada ya michuano hiyoambayo awali ilikuwa ifanyike kwenye uwanja wa Taifa kushindikanaviliibuka vitimbi kibao baina ya hiyo Tiefuefu na timu Simba na Yanga.Kitimbi cha kwanza kilichoibuka ingawa kilionekana kukomaliwa zaidi naYanga huku Simba wakiwa wanajifanya wameuchuna ni kutaka zipewe nafasitatu za kusajili wachezaji wapya.Yanga ndio ilikuwa mstari wa mbele kutishia kujitoa kwenye michuano hiyoendapo isiporuhusiwa kuongeza lakini ghafla bila kujali kwamba awaliwalikuwa wameshakubaliana kwamba kila timu itatumia wachezaji 20wanaocheza Ligi ya ndani, Tiefuefu ikafyata ikakubali wachezaji waongezwengoma ikatulia.“Ninachosema ni hivi mashindano yanachezwa kwenye uwanja wa Taifa,” nikauli ya jamaa mmoja wa Tiefufu ambaye yeye akiwekewa kinasa sautianachojua ni kupayuka tu. Badae nyasi bandia zikashindikana kutolewabandarini kwa muda muafaka akaumbuka. Tumwache.Vitimbi vikaendelea akaibuka Simba, anachosema haendi kwenye uwanja waJamhuri huko Morogoro ngoma ilikohamishiwa mpaka apewe milioni kumi keshikwa mechi zake mbili za kwanza, anachodai Morogoro hakuna mapato.Tiefuefu ikaangaika kukaa na Simbaa… lakini mwisho wa siku waandaajiwakaamua kumaliza ubishi. Klabu zikakutana na wadhamini kwenye kikaoambacho Simba waliwakilishwa na mabosi wawili wakafikia muafaka mashindanoyahamie tena Mwanza.Mashindano yakahamia Mwanza Simba wakageuka maamuzi yao, wakagomahawaendi Kirumba wanataka kubaki Morogoro. Tiefuefu ikaanza kuchachawatena inakaa na Simba kuibembeleza ishiriki.Ndio! sibishi kwamba Tiefuefu inapaswa kukaa na mwanachama wake kuwekasawa baadhi ya ishu za msingi lakini inayumbishwa mno. Aibu gani hii yaunazi wa Simba na Yanga?.Huku ni kuyumbishwa na kushikwa masikio kwa Tiefuefu, haiwezekaniviongozi wenye akili tena sio akili tu timamu, wakubaliane jambo halafubaada ya muda wabadilike kila atake mambo yaende anavyotaka. Basikusingekuwa na haja ya kuwa na chama.Simba hataki kushiriki kwanini mumbeleze? Mmekubaliana kwa kanuni kwa niniTiefuefu msiwe na msimamo mmoja mnabaki kufuata nyayo za rangi tu? Wenyewewanajua wamejitoa kwa nini waacheni.Kwa nini myumbishwe na kikundi cha watu wachache wenye malengo yao? Ndiohay ohayo inafika mwisho wa siku kunafanya Tiefuefu au baadhi ya viongoziwake kudhalilika na hata kutawaliwa na watu wachache.Tiefuefu ifanye kazi kwa kutumia makucha yake, sheria hazikutungwa kuwekwakwenye maktaba au madroo ya hizo. Kila timu kinapaswa kwenda kwa haki ilikuepuka kukandamiza klabu nyingine ambazo siogopi kusema kwamba hazinakauli.………….

Maximo amewatenganisha na ukuta

BALAA hili sasa lashakuwaa..., kubwa kabisa tena zitoo au njama zenutulikimbie jijii.. mwajua ni noma lakini bado mwakandamiza.
Kabisa kabisa tena hata aibu hamuoni mwathubutu kusema bila haya tenamwachekaa.. "karibu tena anko" kwa lipi hilo?.
Mwataka ndondi.. au?.Twazijua sisi mpaka za kijapani nini za kichina china bwana !.Au ndo labda mwataka tuumbuke tusiende haja siee.. tubaki kupiga miyayotuu... kutwaa? Wengine deshi ndio zetu lakini tukizifuma ndio hivyotwaanzia kwenu sababu Pilipili na ndimu Kempiski siku hizi hakuna bwana.

Hakuna! Waziweke za nini wakati wenyewe wanywa vya kwenye makopoyaliyoning'inizwa kwenye hayo majokofu? kule kwetu Ipagala tunaitagaFuriji.Nyie Dizeli na Petroli zakuhusuni nini? au ndio kweli tuaminimwakorofishia viepe? mnatuambia bajeti imekwea, hiyo kitu inahusianaje naPilipili za shingi shirini!Finyango tatu. ..tatu kabisaa... wani...twu...sriii... na maji yakuchemsha (eti mwaita supu?) . Ya kuchemsha kabisamaji tena ya kisima ndio maana matumbo hayatuishi Bongo. mwatuuzia bukuu..!.Huyo wanayemuita Mama Megji mkoba wake umezua balaa huku bongo kila konawimbo ni ugumu wa maisha.Hali imekuwa tete, jua limekuwa kali kupita kiasi mifukoni hata kwa Mamantilie ambako masela walikokuwa wakiponea kwa ugali wa 300 mambo yamekuwasi mambo.Hata vyumba vya buku mbili shin tanu uswahili hakuna tena, zile tabasamukwa washirika wa Mzee wa Kutibua zimepotea na kauli mbiu imekuwa mpakakieleweke.Lakini baadhi yao kama kina Munyuku huko Kijiweni wameanza kuvuta hisia zamaisha ya Vibatari umakondeni sababu muda chi nlefu chafali itawadia.Ndio hivyo! mambo yamebana kasi mpya imegeukia kuunguza waleti sasa naniasubiri kuumbuka auche chuluali.Atabaki nani kwenye hili jiji ambalo siku hizi watuletea mpaka mabinti wakutukogesha kwenye hizo Saluni !Jamaa zinaingia kunyoa sharubu lakini wanagairi wanaanza kukaruza paraili wapate sevisi za hao mabinti mpaka wasinziaaa... kwenyekinanihiii.....kiti. Amah!Kabla sijasahau! kuna jamaa wanakwea pipa leo na kesho twaskiaa...wanakwenda kupiga matizi kwa Wazungu. Dennark na Uswisi.Nyeti alizopata Mzee wa Kutibua laivu toka huyo bosi wao, Mbrazil, MarcioMaximo ni kwamba hao mabwana wanakwenda kusaka makali ya kuwachapa haoWamakonde waite Msumbiji ukijiskia. Huko kwenye dimba la Taifa Septemba9.Oya washkaji hilo shavu hilo. Tumetumia mamilioni ya shilingi ilikuwatengenezea mazingira ya kila aina kuhakikisha mnatupa raha wakubwa,tunataka ushindi tu na tuende Ghana mwakani.Siyo mara ya kwanza hii, miezi fulani fulani hivi siikumbuki tuliwapelekahuko wanakoita Brazil kuwasuka sitaki kufunua mlichofanya baada ya hapo,lakini lazima mtambue tunawapeleka Uzunguni safari hii mkajifue.Hatujawapeleka pikiniki au kushangaa wazungu au magari yenye gorofatunataka mkajifunze na ni nafasi pekee ambazo hazijirudii. Maximoamewatenganisha kwa ukuta mwepesi sana na hao wenzenu huko nje yakikosi. Angalieni wanavyotoka jasho wakiwania hizo nafasi fanyeniupuuzi mjione mastaa abomoe huo ukuta mje mle msoto.Uliyepata nafasi ya kuwa kwenye msafara wa mafunzo jiulize na ufanye kilakinachowezekana kuonyesha umahiri wako Ulaya ni sokoni. tumieni hizomechi za kirafiki kuwahamasisha mawakala wa kimataifa .Kwa jinsi kikosi hicho kilivyo kila mtanzania kama alivyo Mzee wa Kutibuaana imani kwamba Stars itafanya vizuri na kuandika ukurasa mpya katikasoka la Tanzania kwa kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa kuichapaMsumbiji na kufikisha pointi 11. Tujitutumue tuwapige kwanza mengiyatajulikana juu kwa juu.Tumechoka kuwaangalia kina Drogba, Lampard au Essien kwenye kideo,tunataka tumshangilie Haruna Moshi au Saidi Maulid akiwa jijini Accra naFerguson wa Manchesta au Mourhino wa Chelsii akae kwenye sofa na wainiyake awashangae wabongo wanavyokipiga na Cameruni. Alaa?Kila mtu afungue akili yake azingatie maelekezo, hayo mastarehe yapo tumtayakuta, kama ni hela zipo tu hata kabla hamjazaliwa na haziishi milelena mileleni. pigeni kazi washikaji.

Nendeni mkaone ya Sangoma

NAHISI vitu vingi.. vingi.. vingi… vingi, vinginee sivisemi hadharani!Utasema nini wikiendi kama hii ambayo kila kitu segemnege?. Kila mtuanajifanya yuko bize hata katika mambo mengine ambayo hata hayamhusu. Utawaambia nini siku kama hii ambayo kila mtu ni Rais wa Yanga auMwenyekiti wa Simba?. Ni mapambano ya ubabe juu na chini ili mradikieleweke.Jamaa wa mazindiko na wazee wa Kamati za ufundi ndio wakati wa kuneemekakatika harakati za kuhakikisha ushindi unapatikana kwa njia ya Sangoma. Ninoma!.Huko uswazi ardhi za makaburi zinapata taabu kutokana na mishughuliko yahao Makomandoo na wazee wa fitna ambao wamemua kuhama kabisa uraiani etikuweka mambo sawa!.Unashangaa? Siyo makaburini tu hata Kunguru na mayai yake yamekuwa dilimtaani. Wamegeuka zana muhimu kwa wazee wa shughuli baada ya Kuku nafamilia yake kugeuka bidhaa adimu.Hata mateja yaliyokuwa yakinyaka jiti jiti na kupayuka huko kwa MamaZakaria wamesarenda na kuanza msako baada ya kushtukia dili la Kunguru kwaSangoma.Lakini Mzee wa Kutibua alipocheki na Wanyetishaji fulani kutaka kujua kwanini hao Kunguru wamekuwa ishu? Wakajibu eti uzoefu unaonyesha kwambahawana mapozi na wanapenda kujihusisha na majukumu yasiyowahusu . Duhlahaula!.Wabongo? Hakiyanani ni soo. Hakuna tena ufundi wa mpira uwanjani bilamkono wa Sangoma au kuwatoa mhanga hao Kunguru wanaotusafishia hiyoKinondoni huko kwenye jiji la Kandoro. Hao makocha wapo wapo tu kama ushahidi kila kitu kitambooo kamati zawazee wa shughuli zimeshafanya. Utaona mwenyewe.Unabisha? Shauri yako. Wenye mpira wao wanahesabu masaa iwadie hiyo keshomtu mzima aumie kwenye uwanja wa Jamhuri huko wanakoita Morogoro ambakowanataka eti kuwe na Bahari.Watu wazima sema Simba na Yanga ukitaka, wamepenya kwenye hiyo iliyokuwaikiitwa Sita Bora na sasa wamedondokea fainali kumtafuta mbabe wa soka laBongo kwa 2007.Hao jamaa kila mmoja tayari kashapata nafasi ya kushiriki hiyo michuanoya Kimataifa huko mwaka unaokuja lakini ishu ya kesho ndiyo itakayoamuanani aende kwenye hiyo Ligi ya watu wazima. Aah! Sore. Ligi ya Mabingwa namwingine kombe la Shirikisho.Lakini kazeni buti washkaji kesho tunataka kuona soka ya ukweli ukweli, yautu uzima siyo ubabe au misifa ya kijinga. Mzee wa Kutibua na washirikazake wanaibuka kuja kuona soka siyo ngumi.Chezeni mpira hatutaki aibu, onyesheni dira ya kweli kwamba nyinyi ndioSimba na Yanga kweli ambao ni wakongwe wa soka ya Tanzania ambao ni zaidiya hao maswahiba wenu ndio maana mkatinga fainali.Futeni hizi ishu zinazosemwa huku uswahilini kwamba mmebebwa na hao jamaawanaopuliza hizo firimbi. Wanaitwaa… dah! Nitakuambieni badae nimesahau.Wala hatutaki kuona mavurugu yasiyo na maana kama ilivyotokea kwenye hizomechi zilizopita na jamaa fulani fulani kujikuta wakijisaidia ndoo.Ukiacha ishu ya ubingwa, si suala la kuuliza umuhimu wa mechi ya hao jamaakila wanapokutana. Ni mshikemshike ambao huibua mambo mengi.Kila mdau wa soka anataka kuona viongozi wakiwajibika na kutumiaustaarabu wa hali ya juu kuhakikisha mechi inachezwa salama na kila kitukinaenda salama bila rapsha.Viongozi wanapaswa kufanya kazi kama viongozi, si kugeuka makomandoohatutarajii kuona viongozi wenye heshima zao wakisukumana na mashabiki aukupigana au kuendekeza imani za kishirikina kama rekodi zinavyoonyesha.Au hamjiamini? Sasa kiongozi akigeuka mchochezi wa vurugu mnategemea ninikitakachofuata kwa hao wanaojiita Simba damu au Yanga damu.Tubadilike wakubwa. Twendeni kisasa mambo ya kubeba tunguri na zananyingine za Sangoma ni kujiaibisha, waachieni maticha na hao vijana wapigekazi.Kila timu iko fiti na ni nzuri kwa maana ya wachezaji na ushindi unawezakupatikana kwa akili na maarifa ya kiufundi ndani ya dakika 90 za kawaida.Ni jukumu la walio shikilia makali kuhakikisha hata mashabikihawasababishi vurugu zisizo na maana kama ilivyokuwa ikitokea katika mechiza Simba kwenye Ligi Ndogo.Na Polisi nao waache ushabiki. Hayo siyo mambo washkaji ndio hatukataikwamba suala la ushabiki ni haki na uhuru binafsi wa kila raia lakinikatika hili kuweni makini.Acheni hizo ishu wakubwa. Nyendeni uwanjani kuangalia mambo ya usalamamambo ya unazi ni baadaye, jukumu lenu ni usalama si ushabiki.Mzee wa Kutibua hawaonei lakini rekodi zinaonyesha washikaji kwamba majihuwa yanazidi unga. Si tumewashuhudia huko kwenye uwanja wa Taifa hatahapo Morogoro mara kibao tu. Kwanini msiige wanavyofanya wenzenu waRwanda?.

Mambo haya, si mmetaka wenyewe!

JITU zima nimeibuka kama kawa na kibesi kikubwa nikiwa na imani kwamba wanangu mpo fiti ile mbaya kuishambulia vilivyo wikiendi hii.
Kama wapo waliokumbwa japo na tumbo la kuhara basi pole yao, ingawa ni majonzi kupitwa na vyuku vya Idd bwana, lakini ndio ukubwa huo.
Wenye raha zao kuanzia naiti wako mkao wa kutumbua mambo ile mbaya, unaambiwa uswazi mida hii utadhani mashindano, watu hawamaindi masihara bwana, ni makulaji kwa sana sambamba na kujidunga mpaka kuche.
Si unaelewa tena mambo fulani ya mara moja kwa mwaka, madogo na wenyewe wajiskie wako Tizedi siyo kila siku waone mikalangizo kwenye kideo tu. Namna gani vipi bwana,siyo ishu!
Zee la Kutibua bado lipo jijini likizidi kutimba hapa na pale kuhakikisha mambo yanakwenda sawa na waleti linafura kwa ujanja wa mjini na vijana wanakwenda haja kila mara.
Utafanyaje bwana wakati mambo yameshakuwa si mambo na kinazidi kuchafuka kila leo, Uliza Zee la Nyeti litakupa ripoti.
Hujashitukia siku hizi masela walivyokunja ndita huko kwenye hizo daladala, wana haha kurejesha maisha ya enzi za bushi lakini ngoma imekuwa taiti.
Waliojizowelea utasikia ndio Bongo hiyo wanangu, wapo waliopigika na ambao waleti top mkwanja everidei. Ndio maana mwanenu nimeanza kula pozi kimtindo kuinyatia hiyo mnayoita Bigi Blaza.
Mzee wa Kutibia haibuki huko kwenye hilo jumba Sauzi kushangaa magari au taa zinazotumia hewani rodini. Wala hatamani laifu la huyo bwana mdogo wenu Rich na ‘shemeji’ yenu Tatiana, wala! Akyanani tena hizo nanihii za nini wakati mpaka uswazi kwa huyu jamaa hapa kushoto zipo za kukodi kibao!
Mwanenu nataka hilo kwanja, wani hundredi milioni unafikiri masihara mwana! Hapo daladala utanionea kwenye hizo wanaita saitimira tu, mambo ni full kiyoyozi.
Kwa vile hilo shavu bado halijamdondokea Mzee wa Kutibua ngoja auchune kiaina aibuke kwenye ishu zingine zenye maslahi naye kwa sasa kina dada nanihii wasije kumzibia na kujaza masharti tafu. Ila kuna ishu inanizingua nashindwa kuelewa inakuwaje jamaa wana masosi kibao ya mikwanja wanabaki kupiga piga magoti wakiomba kila siku.
Unajua kwanini nasema hivyo? Yanga ninayoijua mimi mzee mzima wa kutibua si klabu ya kumpigia magoti karne hii eti tupe jiwe kadhaa za kulipa mkwanja wa wachezaji.
Unashangaa nini? Kwani hujaskia yule muwezeshaji (kwa kingereza muite sponsa) amemaliza kontracti yake halafu kaishia zake, wakamkimbilia kumpigia magoti awanusuru. Usicheke ni kweli hiyo wala siyo filamu, kawaonea huruma kawapa kama jiwe hamsini hivi.
Hivi kweli nini hiki! Ndio kusema kweli kwamba imefika sehemu Yanga hii hii ninayoijua, imeshindwa kujiendesha pamoja na raslimali zote ilizonazo? Au hawa wanaosema huku nje kwamba kila kiongozi anachuma kwa urefu wake wako sahihi?
Haiwezekani Yanga yenye uwanja, jengo kubwa tena la gorofa iishi maisha kama ya klabu ya Friends Rangers au Kishumundu Fc ambazo zinategemea michango ya jero jero kwa mashabiki ili wapate maji ya kiroba kwenye ndondo.
Sipingi kwamba katiba mbovu inachangia, lakini viongozi wanapaswa kuacha malumbano yasiyo na maana na kuhakikisha wanafanya mambo ya msingi kuendeleza klabu na kuifanya ijiendeshe kisasa zaidi na kujitegemea.
Klabu kama Yanga ina wanazi na wanachama wengi kuliko wateja wa hizo kampuni za bia (kwa mfano Serengeti Bruwarizi) na simu (kwa mfano Vodacom) ambazo zinaendesha timu za Taifa na kudhamini Ligi Kuu inayoshirikisha klabu 14 za Bara.
Haiwezekani viongozi ambao naamini kuwa ni wasomi, nasema naamini! Na wanaoitumikia na kushughulika na majukumu yao kwenye klabu usiku na mchana washindwe kubuni mbinu za kuiendesha klabu kubwa kama Yanga kisomi ingawa kwa kuanzia inawezekana isiwe kwa faida.
Achana na rasilimali zingine ambazo hatuzijui pengine ni siri yao haituhusu, majengo ya klabu yangekarabatiwa kiumakini yangeingiza mamilioni ambayo yangeendesha klabu. Huo uwanja huo…!
Uwanja uliopo Jangwani mkabala na jengo la makao makuu, kwa miaka zaidi ya 20 sasa ni kitega uchumi tosha, unaweza kukarabatiwa na klabu yenyewe au ukakabidhiwa kwa makubaliano maalum kwa wenye uwezo wakaufanya wa kisasa na kutumika kibiashara.
Mechi za ligi zinaweza zikacheza Jangwani na kuiingiza mapato Yanga (kama Aseno, Chelsii zinavyovuna Emiretsi na Stanfodi Briji) ikaishi yenyewe na hata kama itakuwa na wadhamini wachache haitawapigia magoti kama ilivyo sasa.
Hakuna ambacho kingeshindikana endapo viongozi wangeharakisha kufanya mabadiliko ya katiba kwa kushirikiana na wanachama na kufanya mambo kuwa ya kisasa zaidi na kila mmoja kuchangia maendeleo ya klabu kwa ukaribu zaidi. Wanachama na nyie muwe makini si kila mtu anafaa kuwa kiongozi, msiangalie maslahi binafsi.
Cheameni Madega na jopo lako mnapaswa kuharakisha baadhi ya mambo, haiwezekani mwanachama akachangia buku kwa mwezi halafu ukategemea mabadiliko. Viongozi wanaweza kujitetea kwamba ndio wanahangaikia mabadiliko ya katiba, evuri dei?
Wanachama na wenyewe wanapaswa kuamka na kujua kwamba hii ni karne mpya, wasiendeshe mambo kama tuko mwaka themanini, mambo ya kupigia magoti ‘wenye ndevu’ yamepitwa na wakati. Hata ujanja ujanja wa kudokoa hela za wadhamini kwa baadhi ya viongozi uachwe, ni aibu.