Friday, November 2, 2007

Maximo sawa bwana-Ndabila


MSHAMBULIAJI tegemeo wa Prisons, Yona Ndabila amesema hana bahati na timu ya Taifa na wala hadhani kwamba anaweza akawemo katika miaka ya hivikaribuni.

Kauli ya mchezaji huyo imekuja siku chache baada ya kocha Marcio Maximo kutangaza kikosi cha Chalenji huku akiwa hayumo licha ya wadau wengi kushinikiza awemo.

“Timu mi naona ni nzuri, lakini mi naona kama sina bahati kabisa kipindi hiki kwa jinsi mambo ninavyoyaona,”alisema mchezaji huyo mwenye mabao manne kwenye Ligi Kuu ya Bara inayoendelea.

“Wakati huu ndio naona nipo kwenye fomu sana na ndio ilikuwa kipindi changu cha kulitumikia taifa kwa kila hali.

“Lakini ndio hivyo, labda ipo siku hii ni kazi yangu ngoja tupambane na Ligi Kuu kwanza tuone,”aliongeza mchezaji huyo mfupi kiasi mwenye maneno mengi.

No comments: