Friday, November 2, 2007

Wa mnyama saba hawamo kambini

WACHEZAJI saba tegemeo wa Simba ya Dar es Salaam hawamo kwenye kambi ya mazoezi ya timu hiyo mjini Morogoro.

Simba yenye pointi 15 ikishikilia nafasi ya nane inacheza na Polisi Dodoma kesho mjini Dodoma katika mechi ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara.

Habari toka ndani ya kambi hiyo zinasema kuwa wachezaji hao watano kati yao waliondoka kambini juzi mchana na jana walionekana katika mitaa mbalimbali za Dar es Salaam wakiendelea na mitikasi yao.

Wachezaji ambao waliondoka kwenye kambi hiyo juzi ni Joseph Kaniki, Haruna Moshi ‘Boban’, Mussa Hassan Mgosi, Soud Abdallah,Nurdin Bakar na Moses Odhiambo wakati Akilimali Yahya bado hajapona.

No comments: