Friday, October 12, 2007

Mambo haya, si mmetaka wenyewe!

JITU zima nimeibuka kama kawa na kibesi kikubwa nikiwa na imani kwamba wanangu mpo fiti ile mbaya kuishambulia vilivyo wikiendi hii.
Kama wapo waliokumbwa japo na tumbo la kuhara basi pole yao, ingawa ni majonzi kupitwa na vyuku vya Idd bwana, lakini ndio ukubwa huo.
Wenye raha zao kuanzia naiti wako mkao wa kutumbua mambo ile mbaya, unaambiwa uswazi mida hii utadhani mashindano, watu hawamaindi masihara bwana, ni makulaji kwa sana sambamba na kujidunga mpaka kuche.
Si unaelewa tena mambo fulani ya mara moja kwa mwaka, madogo na wenyewe wajiskie wako Tizedi siyo kila siku waone mikalangizo kwenye kideo tu. Namna gani vipi bwana,siyo ishu!
Zee la Kutibua bado lipo jijini likizidi kutimba hapa na pale kuhakikisha mambo yanakwenda sawa na waleti linafura kwa ujanja wa mjini na vijana wanakwenda haja kila mara.
Utafanyaje bwana wakati mambo yameshakuwa si mambo na kinazidi kuchafuka kila leo, Uliza Zee la Nyeti litakupa ripoti.
Hujashitukia siku hizi masela walivyokunja ndita huko kwenye hizo daladala, wana haha kurejesha maisha ya enzi za bushi lakini ngoma imekuwa taiti.
Waliojizowelea utasikia ndio Bongo hiyo wanangu, wapo waliopigika na ambao waleti top mkwanja everidei. Ndio maana mwanenu nimeanza kula pozi kimtindo kuinyatia hiyo mnayoita Bigi Blaza.
Mzee wa Kutibia haibuki huko kwenye hilo jumba Sauzi kushangaa magari au taa zinazotumia hewani rodini. Wala hatamani laifu la huyo bwana mdogo wenu Rich na ‘shemeji’ yenu Tatiana, wala! Akyanani tena hizo nanihii za nini wakati mpaka uswazi kwa huyu jamaa hapa kushoto zipo za kukodi kibao!
Mwanenu nataka hilo kwanja, wani hundredi milioni unafikiri masihara mwana! Hapo daladala utanionea kwenye hizo wanaita saitimira tu, mambo ni full kiyoyozi.
Kwa vile hilo shavu bado halijamdondokea Mzee wa Kutibua ngoja auchune kiaina aibuke kwenye ishu zingine zenye maslahi naye kwa sasa kina dada nanihii wasije kumzibia na kujaza masharti tafu. Ila kuna ishu inanizingua nashindwa kuelewa inakuwaje jamaa wana masosi kibao ya mikwanja wanabaki kupiga piga magoti wakiomba kila siku.
Unajua kwanini nasema hivyo? Yanga ninayoijua mimi mzee mzima wa kutibua si klabu ya kumpigia magoti karne hii eti tupe jiwe kadhaa za kulipa mkwanja wa wachezaji.
Unashangaa nini? Kwani hujaskia yule muwezeshaji (kwa kingereza muite sponsa) amemaliza kontracti yake halafu kaishia zake, wakamkimbilia kumpigia magoti awanusuru. Usicheke ni kweli hiyo wala siyo filamu, kawaonea huruma kawapa kama jiwe hamsini hivi.
Hivi kweli nini hiki! Ndio kusema kweli kwamba imefika sehemu Yanga hii hii ninayoijua, imeshindwa kujiendesha pamoja na raslimali zote ilizonazo? Au hawa wanaosema huku nje kwamba kila kiongozi anachuma kwa urefu wake wako sahihi?
Haiwezekani Yanga yenye uwanja, jengo kubwa tena la gorofa iishi maisha kama ya klabu ya Friends Rangers au Kishumundu Fc ambazo zinategemea michango ya jero jero kwa mashabiki ili wapate maji ya kiroba kwenye ndondo.
Sipingi kwamba katiba mbovu inachangia, lakini viongozi wanapaswa kuacha malumbano yasiyo na maana na kuhakikisha wanafanya mambo ya msingi kuendeleza klabu na kuifanya ijiendeshe kisasa zaidi na kujitegemea.
Klabu kama Yanga ina wanazi na wanachama wengi kuliko wateja wa hizo kampuni za bia (kwa mfano Serengeti Bruwarizi) na simu (kwa mfano Vodacom) ambazo zinaendesha timu za Taifa na kudhamini Ligi Kuu inayoshirikisha klabu 14 za Bara.
Haiwezekani viongozi ambao naamini kuwa ni wasomi, nasema naamini! Na wanaoitumikia na kushughulika na majukumu yao kwenye klabu usiku na mchana washindwe kubuni mbinu za kuiendesha klabu kubwa kama Yanga kisomi ingawa kwa kuanzia inawezekana isiwe kwa faida.
Achana na rasilimali zingine ambazo hatuzijui pengine ni siri yao haituhusu, majengo ya klabu yangekarabatiwa kiumakini yangeingiza mamilioni ambayo yangeendesha klabu. Huo uwanja huo…!
Uwanja uliopo Jangwani mkabala na jengo la makao makuu, kwa miaka zaidi ya 20 sasa ni kitega uchumi tosha, unaweza kukarabatiwa na klabu yenyewe au ukakabidhiwa kwa makubaliano maalum kwa wenye uwezo wakaufanya wa kisasa na kutumika kibiashara.
Mechi za ligi zinaweza zikacheza Jangwani na kuiingiza mapato Yanga (kama Aseno, Chelsii zinavyovuna Emiretsi na Stanfodi Briji) ikaishi yenyewe na hata kama itakuwa na wadhamini wachache haitawapigia magoti kama ilivyo sasa.
Hakuna ambacho kingeshindikana endapo viongozi wangeharakisha kufanya mabadiliko ya katiba kwa kushirikiana na wanachama na kufanya mambo kuwa ya kisasa zaidi na kila mmoja kuchangia maendeleo ya klabu kwa ukaribu zaidi. Wanachama na nyie muwe makini si kila mtu anafaa kuwa kiongozi, msiangalie maslahi binafsi.
Cheameni Madega na jopo lako mnapaswa kuharakisha baadhi ya mambo, haiwezekani mwanachama akachangia buku kwa mwezi halafu ukategemea mabadiliko. Viongozi wanaweza kujitetea kwamba ndio wanahangaikia mabadiliko ya katiba, evuri dei?
Wanachama na wenyewe wanapaswa kuamka na kujua kwamba hii ni karne mpya, wasiendeshe mambo kama tuko mwaka themanini, mambo ya kupigia magoti ‘wenye ndevu’ yamepitwa na wakati. Hata ujanja ujanja wa kudokoa hela za wadhamini kwa baadhi ya viongozi uachwe, ni aibu.

No comments: