Friday, October 26, 2007

Mukandila Tshitenge Kabanda:Im very sorry Yanga


Kaka kuna pua ya mtu nini?


ENGLAND ilivyofungwa wiki chache zilizopita na Russia 2-1 kwenye michuano ya kuwania kufuzu Euro 2008, nahodha wao Steven Gerrard aliwaambia Waingereza “samahani” huku kocha wake, Steve Mclaren akisema "Mnilaumu mimi."

Lakini kwa mara ya kwanza kwa mastaa wa kimataifa nchini Tanzania, mshambuliaji ghali wa Yanga, Mukandila Tshitenge Kabanda amewaomba radhi maelfu ya mashabiki wa klabu yake kwa kushindwa kuifunga Simba Jumatano mjini Morogoro kwenye pambano la Ligi Kuu ya Bara.

Yanga licha ya Sh milioni 50 ilizokuwa imepewa na mfadhili wake, Yusuf Manji ili iifunge Simba ilishindwa kutekeleza azma hiyo na kujikuta ikikubali kipigo cha bao 1-0 lililofungwa na Ulimboka Mwakingwe dakika ya 30 kwa shuti kali ambalo lilimpita kwapani kipa wa Stars, Ivo Mapunda.

Kabanda, ambaye aliumia baada ya kugongana na kipa wa Simba, Juma Kaseja alisema kuwa alikuwa amepania kuipa ushindi yake na alikuwa na tamaa ya mabao lakini mambo yakamuendea vibaya.

“Naomba wanisamehe tu kwa kushindwa kuwapa ushindi na kufunga magoli, sikufanya kusudi nilikuwa na tamaa sana na hamu ya kufunga magoli,” alisema Kabanda(mwenye rasta anayeangalia mbele) ambaye kabla ya kutua Yanga alikuwa APR ya Rwanda.

“Nilikuwa nimepania kucheza kwa nguvu zangu zote kuhakikisha kwamba timu yangu inashinda kwa vile nilikuwa najua ndio zawadi pekee ya mashabiki na viongozi wangu.

“Lakini hatukufanya kusudi, naomba watuamini ligi bado ni ndefu hii ni mechi ya kwanza tumekutana na hawa Simba tutakutana nao bado kuna mechi nyingine tukiwakuta tutawafunga tu, tutakuwa tumebadilika zaidi hakuna kukata tamaa.

“Na mimi na miaka miwili ya kukaa Yanga, sasa bado sijamaliza hata mmoja wa kwanza nitabadilika tu na nitaanza kufunga magoli, nimepania sana lakini bado sijapata bahati ya kutekeleza azma yangu.
Aliumiaje? : Kaseja aliruka juu wakati anaokoa mpira akanigonga na goti kwenye shingo, niliumia sana yaani nilisikia kichwa kinauma, shingo inauma, kizunguzungu ndio maana wakanipeleka hospitali.
“Siwezi kusema kwamba ni kusudi, siwezi kujua lakini mimi namuamini Mungu ndie anajua na naamini kwamba ni hali ya mchezo tuu imetokea bahati mbaya na inaweza kumtokea mtu yoyote yule anayecheza nafasi kama yangu.

No comments: