Friday, October 12, 2007

Necha kaula kinoma shavuuu nhihaaaaaaaaaaa!

MSANII maarufu wa muziki wa Rap nchini, Juma Kassim ‘Nature’ amefanikiwa kuibuka mshindi wa tuzo za Video Bora ya Channel O kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.Katika tuzo hizo zilizofanyika jana, Nature alifanikiwa kuwashinda wasanii wengine watano kutoka Kenya na Uganda na kuibuka na ushindi huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na Watanzania wengi.Aliochuana nao katika kitengo cha video bora ya Afrika Mashariki huku yeye akitumia wimbo wake wa ‘Mugambo’, walikuwa ni E.A.B.C – Kube, IDA - Make it Hot, Nameless – Sinzia, Wyre - Make A Choice (wote kutoka Kenya) huku Peter Miles - Love akiwa anatokea Uganda.Mashabiki kadhaa walijitokeza jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam kumlaki Nature ambaye aliongozana na msanii mwenzake Rich One kwenda katika tuzo hizo. Baadhi ya mashabiki hao walikuwa wakisukuma gari alilokuwa amepanda Nature baada ya kuwasili kuonyesha furaha nyao kwa msanii huyo kipenzi cha wengi.Hii ni mara ya pili kwa Nature kuwania tuzo hizo na pia aliwahi kuwania tuzo za MTV kupitia wimbo huop lakini akaambulia patupu.Msanii mwingine wa Tanzania ambaye amewahi kushinda tuzo ya Channel O ni Lady Jaydee kupitia nyimbo zilizokuwa katika albamu ya Machozi na Binti.Kwa sasa Nature ndiye kiongozi wa kundi la Wanaume Halisi baada ya kutengana na wenzao katika kundi la Wanaume TMK ambao nao kwa sasa wanajulikana kama Wanaume Original.Nature ni kati ya wasanii wanaokubalika kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kuimba aina tofauti ya muziki na wimbo wa ‘Mugambo’ ameuimba katika miondoko ya Kwaito ambayo ni maarufu sana Afrika Kusini.Ushindi wake unakuwa ni mwanzo wa ndoto zake na amewahi kutangaza kuwa kushinda tuzo hasa za nje ya Tanzania imekuwa ni moja ya ndoto kubwa ndiyo maana alijisikia vibaya aliposhindwa kutwaa tuzo ya MTV lakini hakutakata tamaa.Awali, Nature alikuwa na hofu huenda ingekuwa vigumu kushinda tuzo hiyo kutokana kuwa na Wakenya wengi ambao wengi pia waliamini huenda ndiyo walikuwa na nafasi kubwa zaidi lakini ‘akawapasua’ na kuibuka kidedea.

No comments: