Friday, October 26, 2007

Hawa Prisons ni noma wanabonda tuuuu


You Guys mko siriaz au ndio mnatuyeyusha


LICHA ya kupoteza mechi moja na kutoa sare mbili ugenini huku ikiendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Bara, Prisons imedhihirisha kwamba bado ni bora kuliko timu yoyote.

Klabu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Magereza katika mechi zote kumi ilizocheza hadi sasa inashabihiana na Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Toto Africa na Coastal Union kwa kitu kimoja tu; mabao nane ya kufungwa.

Prisons imeshinda mechi saba, sare mbili na kupoteza mchezo mmoja rekodi ambayo haipo kwa timu yoyote inayoshiriki michuano hiyo hata Simba na Yanga zenye wachezaji ghali na maarufu.
Mbali na hilo, Prisons ambayo kocha wake ni Juma Mwambusi, imepachika mabao 18 ambayo hayajakaribiwa na timu yoyote labda Polisi Dodoma na Kagera Sugar zenye mabao 10 kila moja.
Timu hiyo ambaye imekuwa ikisifika zaidi kwenye upande wa kiungo, ina pointi 23 ambazo inaweza kuziongeza itakapocheza na Moro United keshokutwa.

Washambuliaji wake, Oswald Morris anaongoza kwa ufungaji akiwa na mabao sita, huku Yona Ndabila na Said Mtupa wakiwa na mabao manne pia, sawa na Mike Katende wa Kagera Sugar.

Wachezaji wengi wa Simba na Yanga wanadai kuwa timu hiyo ilikuwa ikishinda kwa vile imecheza mechi nyingi kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Sokoine, Mbeya, lakini sasa itaanza kupata vipigo ikianza kutoka ugenini.

Tayari Prisons imepoteza mchezo moja dhidi ya Kagera Sugar.

No comments: